Madiwani wilayani
Hanang’ mkoani Manyara wamelalamikia upungufu mkubwa wa Dawa na ukosefu
wa
huduma za Afya katika Hospitali ya Tumaini iliyoko maeneo ya Katesh
wilaya ya
Hanang’ mkoani Manyara.
Malalmiko hayo
yamekuja kutoka kwa baadhi ya madiwani wa Halmashauri hiyo kwenye kikao
cha
Baraza la madiwani la kujadili taarifa ya utekelezaji kwa kipindi cha
robo
mwaka ya pili Oktoba hadi Desemba 2012.
Naye
Diwani
wa Kata Endagaw Hassan Hilbagroy aliuliza kuwa sifa ya vituo vya Afya ni
zipi?ni mlundikano wa wagonjwa au ni mahali pa kupatia tiba ?wakati
akichangia
hoja yake kuhusu ukosefu wa huduma stahili katika Hospitali na vituo vya
afya
wilayani hapo.
Alisema kuwa
kuwasilisha kwa masikitiko hayo kwa kusema mgonjwa anafika kwenye kituo
cha
Afya atakaa hapo akisubiri kumwona mganga kwa zaidi ya masaa
matatu,akiandikiwa
dawa anaenda tena kukaa kwa masaa matatu kumsubiri mtoa dawa, mtoa dawa
akifika
anasema dawa hakuna,huu ni mchezo gani.
Naye mganga mkuu wa
Wilaya ya Hanang’ Dr Philemon Kiambile wakati akijibu hoja hiyo kwa
madiwani
hao amekiri kuwepo kwa upungufu wa Dawa na kueleza kuwa upungufu huo
umetokana
na uchangiaji mdogo wa mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) .
Aidha kijibu hoja
hizo kwa madiwani hao alisisitiza kuwa tayari Halmashauri ya wilaya hiyo
imepokea ruzuku kutoka Serikalini ya kiasi cha Tshs milioni 44 kwa ajili
ya
ununuzi ya Dawa ambazo zitasambazwa kwenye vituo vyote vya Afya pamoja
na
Zahanati.
Kwa upande wake
Mkurugenzi wa Wilaya ya Hanang’ Filex Mabula ameagiza iundwe timu
itakayofanya
ununuzi wa dawa kwa uwazi na kusambazwa kwa uwazi ili hata wananchi
wajue
kwamba kituo kina madawa.
Alisema kuwa
wanataka ununuzi wa madawa ufanyike kwa uwazi ili hata wananchi wao
wajue dawa
kwenye kituo chao zipo,hata akienda kutibiwa akiambiwa hakuna dawa awe
na
maswali ya kuhoji yameenda wapi iwapo ni wiki tu tangu ziletwe.
