SAKATA LA KUBOMOLEWA NYUMBA NA MGAHAWA MTAA WA OHIO

 Rubani Mstaafu wa Ndege za Serikali, Felix Henry Kileo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana juu ya tukio la kuvinjiwa nyumba namba 15 aliyokuwa akiishi na kufanya biashara katika kitalu namba 223/50 kilichopo mtaa wa Ohio jijini humo. Kwa Mujibu Wa wakala wa Majengo wa Serikali (TBA) Kiwanja hicho kinamilikiwa na Benki ya Uwekezaji Tanzania (TIB) na Benki hiyo inataraji kujenga Makao makuu ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB). 

Rubani huyu alidai kitendo cha kubomolewa nyumba yake ni cha kinyama kwani yeye alikuwa mtumishi wa serikali kama rubani na katika kipindi chote cha utumishi wake hakuwahi hata siku moja kupata ajali hata pancha akiendesha Viongozi kama Marais.

 
Vitu vikiwa nje 
Vyombo vilivyokuwa vikitumika upande wa Biashara vikiwa nje.Mgahawa ulikuwa maarufu kama Kwa Mama.

Hizi ndio barua zenye maelezo kamili juu ya sababu ya kubomolewa nyumba hizo na lengo ni nini la Ubomoaji huo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo