KATI KATI NI MWENYEKITI WA CCM
ALIYEMALIZA MUDA WAKE 2012 WILAYA YA MBEYA VIJIJINI WILLIUM SIMWALI
BAADHI ya viongozi wa Chama cha
Mapinduzi (CCM) na baadhi ya jumuiya
zake ikiwemo ile ya vijana (UVCCM) mkoani Mbeya wanatarajiwa kuhamishwa
na
uchaguzi kurudiwa baada ya kubainika na kulalamikiwa kujiingiza katika
vitendo
vya kuomba, kupokea na kutoa rushwa.
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya chama hicho, zimeeleza kuwa
baada ya uchaguzi huo baadhi ya wanachama walipeleka malalamiko ngazi za
juu za
chama na utafiti ukawa unaendelea.
Imeelezwa kuwa waliolalamikiwa na kuhojiwa ni pamoja na makatibu
wa chama hicho ngazi za wilaya na baadhi ya wagombea wa nafasi
mbalimbali na
baadhi wameshindwa kujieleza.
Mmoja wa kiongozi wa UVCCM, anadaiwa kutumia cheti cha ubatizo
ambacho hakiendani na jina lake hali ambayo inatafsiriwa kuwa alipita na
kuchaguliwa isivyo halali na kwamba kuna wengine ambao wanajihusisha na
uimarishaji wa makundi ya wanaohitaji kugombea nafasi ya Rais mwaka
2015.
Katibu wa CCM katika wilaya ya Mbeya Vijijini ni mmoja wa
makatibu ambao wanatajwa kuwa anaweza kuhamishwa kutokana na malalamiko
kadhaa
ya wanachama wa wilaya hiyo.
Hata hivyo, uchunguzi uliofanywa na mtandao huu, umebaini kuwa
baadhi ya waliotangazwa kushinda katika nafasi kadhaa za chama hicho
katika
wilaya hiyo ni batili kwasababu wagombea ambao kura zilitosha hawakuweza
kutangazwa kutokana na kutoweza kuchangia fedha zilizodaiwa kuwa ni za
maandalizi ya uchaguzi