PROFESA JAY ADAIWA KUMTAPELI PROMOTA WA MOMBASA- KENYA


Kwa mujibu wa gazeti la The Star ka nchini Kenya, rapper Joseph Haule aka r Profesa Jay hivi karibuni aliingia kwenye mgogoro na promoter wa mjini Mombasa Kenya aliyemchukua kufanya show. Prof alikuwa amechukuliwa kufanya show mbili siku ya Christmas kwenye kumbi za Jamboree Resort na Quetu Beach Resort.


Inavyodaiwa Profesa Jay hakuwa amelipwa fedha zote kwa show ya pili na hivyo alipewa camera aina ya Nikon D3000 kama rehani.Baada ya show, Prof aliondoka nchini Kenya na crew yake na kuibeba kamera hiyo. Sasa waandaaji hao wanadai kuwa walimpatia Prof hela yake iliyokuwa imesalia.

Issue hiyo imekuwa kubwa kiasi ambacho passport ya mpambe aliyekuwa amesafiri na Jay nchini humo imeshikiliwa ili asiondoke.Waandaaji wanadai kuwa walimlipa Profesa Jay shilingi 252,000 za Kenya ambazo ni zaidi hata ya fedha walizokuwa wamekubaliana na sasa wanataka warudishiwe fedha yao.

Polisi wanashughulikia kesi hiyo na Prof aliyekuwa ameingia makubaliano ya show nyingine katika ukumbi wa Jamboree December 31 aliitosa show hiyo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo