Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akisoma hotuba yake wakati
alipokuwa mgeni rasmi kwenye Mahafali ya Kidato cha Sita kwa Jumuiya ya
Wanafunzi wa Kiislamu wa Shule ya Sekondari ya Tambaza. Mahafali hayo
yamefanyika leo, katika shule hiyo ya Tambaza jijini Dar es Salaam.
Katika hotuba yake Mama Asha amewahasa vijana hususan wanafunzi hao
waliohitimu masomo kutokukubali kutumika na watu wenye maslahi binafsi
na kujikuwa wakisababisha uvunjifu wa amani. Aidha amewataka
kutojihusisha na makundi yanayochochea uvunjifu wa amani bila kujitambua
wafanyalo, badala yake amewambo kuwa wakipima kila wanaloambiwa kuwa
linamaslahi na dini yao ama maslahi kwa jamii na taifa kwa ujumla. Picha
Zote na www.sufianimafoto.blogspot.com
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akimkabidhi Cheti mmoja
wa wahitimu wa Kidato cha Sita, Latifah Nuhu, wakati wa sherehe za
mahafali ya Kidato cha Sita kwa Jumuiya ya Wanafunzi wa Kiislamu wa
Shule ya Sekondari ya Tambaza. Mahafali hayo yamefanyika leo,
katika shule hiyo ya Tambaza jijini Dar es Salaam.
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akimkabidhi Cheti mmoja
wa wahitimu wa Kidato cha Sita, Mwinga Gwao, wakati wa sherehe za
mahafali ya Kidato cha Sita kwa Jumuiya ya Wanafunzi wa Kiislamu wa
Shule ya Sekondari ya Tambaza. Mahafali hayo yamefanyika leo,
katika shule hiyo ya Tambaza jijini Dar es Salaam.
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akimkabidhi zawadi mhitimu wa
Kidato cha Sita, Zuhura Azmin, kwa kuwa mmoja kati ya waliofanikisha
sherehe za mahafali ya Kidato cha Sita kwa Jumuiya ya Wanafunzi wa
Kiislamu wa Shule ya Sekondari ya Tambaza. Mahafali hayo yamefanyika
leo, katika shule hiyo ya Tambaza jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wahitimu wa kike wakiwa katika mahafali hayo leo.
Baadhi ya wahitimu wa kiume, wakiwa katika mahafali hayo leo.
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akimkabidhi Cheti mmoja
wa wahitimu wa Kidato cha Sita, Khadija Hassan, wakati wa sherehe za
mahafali ya Kidato cha Sita kwa Jumuiya ya Wanafunzi wa Kiislamu wa
Shule ya Sekondari ya Tambaza. Mahafali hayo yamefanyika leo,
katika shule hiyo ya Tambaza jijini Dar es Salaam.
Dua baada ya shughuli hiyo kukamilika.
Mama Asha, akiwa katika picha ya
pamoja ya kumbukumbu na baadhi ya wanafunzi wahitimu wa kidato cha sita,
baada ya zoezi la kugawa vyeti kwa wahitimu.