Mkurugenzi wa Huduma za Usafiri wa Wizara ya
Uchukuzi, Peter Lupatu, akikata utepe kuzindua Safari za Ndege za
Shirika la Precision Air za Mbeya kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Songwe. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Precision Air, Michael
Shirima.
Mkurugenzi wa Huduma za Usafiri kutoka
Wizara ya Uchukuzi, Peter Lupatu, akishuka kutoka katika ndege ya
shirika la Precision Air wakati wa uzinduzi wa Safari za Mbeya – Dar
kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe kabla ya kukata utepe
kuzindua safari hizo. Nyuma yake ni Mwenyekiti wa Bodi ya shirika hilo,
Michael Shirima.
Mwenyekiti wa Bodi ya Precision Air (PW),
Michael Shirima, (Kushoto) akiteta jambo na abiria wa kwanza kununua
tiketi ya safari ya Mbeya wakati wa uzinduzi wa Precision Air wa njia ya Mbeya –
Dar, Bw. Alfred Mwambeleko Jumatano hii.
Mzee akisaidiwa kupanda
ndege, ambaye ni mkazi wa mkoani Mbeya wakati wa uzinduzi wa Safari za
Ndege za Shirika la Precision Air za Mbeya – Dar uliofanyika Jumatano
hii kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe uliofanyiwa
marekebisho kutumika kwa safari za kimataifa.