Mwanamke
anayejulikana kwa jina Mwanaisha Idd umri wa miaka 25 mkulima wa kijiji
cha Kichameda amekutwa ameuwawa kwenye korongo eneo la Mrara
mjini Babati mkoani Manyara.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi wa mkoa wa manyara Akili
Mpwapwa
alisema kuwa tukio hilo lilitokea januari 10 mwaka huu majira ya saa 11
jioni
marehemu alikutwa amekufa korongoni huku mwili wake ukiwa uchi huku nguo
zake
zikiwa pembeni mwake.
Aidha
aliongeza kuwa mwili wa marehemu Mwanaisha umekutwa amechuchumaa kama
akisujudu
huku akiwa ameingiliwa kimaumbile pande zote mbili hakuwa na jereha
lolote
lile.
Kamanda
Mpwapwa aliendelea kusema kuwa kutokana na tukio hilo uchunguzi
umefanywa na
kuweza kumkamata mtu mmoja ambaye alizaa na marehemu watoto wawili
anayeitwa
John Mathayo umri wa miaka 35,mkulima wa kijiji cha Kichameda.
Alisema
kuwa John Mathayo alikuwa na mahusiano na marehemu mwanaisha ambapo yupo
mtuhumiwa amekamatwa na yupo ndini kwaajili uchunguzi, atafikishwa
mahakamani upelelezi ukikamilika.