WATU watatu wamefikishwa Mahakamani
Mkoa wa Manyara wakishtakiwa kwa kosa la uhujumu uchumi kwa kuua tembo
na
kosa la jinai la kukutwa na silaha wakati wakiwinda wanyamapori katika
hifadhi
ya Tarangire.
Aidha wakisomewa mashtaka hayo mjini
Babati mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Rashid
Chaungu, mwendesha
mashtaka Linus Bugaba alisema kuwa washtakiwa hao wanadaiwa kutenda
makosa hayo Agosti 27 mwaka jana.
Amewataja washtakiwa hao kuwa ni Gidabijo
Gidabungeta
(35) mkazi wa Makuyuni mkoani Arusha,Mahaya Gidamude (26) na Masanja
Bajuta
(26) wote wakazi wa kijiji cha Mdori wilayani Babati mkoani Manyara.
Aliendelea kusema kuwa katika kesi namba
21/2012 ya
uhujumu uchumi washtakiwa hao wanadaiwa kumuua tembo mmoja na kisha
kuchukua
pembe zake na kesi ya jinai namba 441/2012 wanadaiwa kukutwa na silaha
ya
bunduki na risasi.
Alisema kuwa kwenye
shtaka la kwanza ya uhujumu uchumi,washitakiwa hao wanadaiwa kukutwa na
nyara
za Serikali baada ya kumuua tembo mmoja na kuchukua pembe zake ambazo
juzi
zililetwa Mahakamani hapo kama kielelezo.
Bugaba alibainisha kuwa shtaka la pili
linalowakabili washtakiwa hao ni kukutwa kwenye tukio hilo hifadhi ya
Tarangire
wakiwa na silaha aina ya Rifle 404 risasi mbili za 404 na maganda
yake,mkuki na
kielelezo cha nguo (shuka za kibarabaig).
Kwa upande wao washtakiwa
hao wamekana makosa hayo na wapo nje kwa dhamana hadi Januari 31 mwaka
huu
ambapo kesi ya jinai upande wa mashtaka wataendelea na ushahi wao pamoja
na
kuonyesha vielelezo.
Aidha Bugaba alimalizia kwa kusema
kuwa kosa la uhujumu uchumi lipo kwenye hatua ya kutajwa kwani
wanasubiri kibali kutoka kwa mwanasheria wa Serikali na itajawa Januari
31
mwaka huu.