Agosti 27, Kiongozi mmoja wa dini ya Kiislamu nchini Kenya, Shehe Aboud
Rogo
aliuawa kwa kupigwa risasi ndani ya gari lake mjini Mombasa.
Vijana wa
Kiislamu
katika mji huo wa ukanda wa Pwani walianzisha ghasia mara moja baada ya
tukio
hilo ambapo waliharibu na kuchoma moto makanisa katika vurugu za kiimani
mbaya
zaidi kuwahi kutokea katika nchi Kenya. Viongozi wa dini toka pande zote
mbili
walijaribu kwa kila hali kuwasihi wafuasi wao na kurejesha tena utulivu
katika
eno hilo.
Lakini tukio hili ni la pekee zaidi ambapo
lilishuhudia uvumilivu wa dini tofauti ukiwa umejaribiwa kwa kiwango cha
juu
kwa mwaka 2012 kwa nchi za Kenya na Tanzania.
Mapema,Jumapili
ya Julai mosi,mabomu mawili yalirushwa kwa waumini waliokuwa wanasali
katika
makanisa mawili tofauti, enee la Garisa,katika mkoa wa Kaskazini
Mashariki
unaopakana na nchi ya Somalia. Jumla ya watu 17 walikufa, wakiwemo
polisi
wawili waliokuwa wanalinda moja ya makanisa hayo.Pia waumini 60
walijeruhiwa.
Kiongozi
huyo wa Kiislamu, Shehe Rogo aliyeuawa, awali alitamka wakati wa swala
ya
Ijumaa msikitini mjini Mombasa kufuatia mashambulizi hayo ya Garisa
kwamba
tukio hilo lilifanywa na Waislamu kulipiza kisasi. Polisi hawakumkamata.
Wakati tukio
hilo lilitoa ishara ya Waislamu kuishi kwa mashaka na Wakristu nchini
Kenya,
hali kama hiyo ya mashambulizi ya moja kwa moja haijawahi kutokea katika
kipindi cha miaka lukuki.
Wiki
tatu baada ya mashambulio ya Garisa,polisi nao walikamata mabomu
yaliyokuwa
yanadaiwa kuwa yangetumika kulipua kanisa Katoliki la Assumption of
Mary,
katika Parokia ya Umoja, jijini Nairobi. Watu wawili waliokamatwa na
mabomu
hayo waliripotiwa kuwa waliyaingiza mabomu hayo kutoka nchi moja jirani
na
Kenya.
Kwa upande
mwingine wa mgawanyiko huo kwa misingi ya kidini, kulikuwepo pia kupamba
kwa
uhasama miongoni mwa jamii za Waislamu wenyewe.Jarida la kila wiki
linalochapishwa na Jamia Mosque mjini Nairobi la The Friday
Bulletin,liliripoti
Agosti kwamba waislamu wenye imani kali walibomoa msikiti mmoja katika
wilaya
Kajiado,kumwagia kinyesi msikini na kuchoma moto nakala za Korani,
Kitabu
Kitakatifu cha Waislamu. Msikiti huo ulikuwa unajengwa eneo la Olkejuado
High
School, ulikuwa unakaribia kukamilika.
Katika tukio la pili,Mwalimu Mkuu wa Kangeta
High
School, Meru aliwatimua wanafunzi 15 baada ya kusisitiza kufunga wakati
wa
mwezi wa Ramadhani, hivyo kwenda kinyume na amri ya mkuu wao wa shule.
Kujihusisha kwa Kenya, kijeshi nchini Somalia
tangu
Oktoba 2011, ambako jeshi la nchi hiyo linapambana na kundi la
wanamgambo la Al
Shabaab lilifungulia kuliongeza kwa matukio ya kigaidi.Mashambulio hayo
kwa
kiasi kikubwa yalifanya hali ya uhasama kuwa mbaya zaidi 2012 kati ya
dini hizo
mbili kuu nchini Kenya za Kikristu na Kiislamu.
Nchini Tanzania, Shehe Ponda Issa Ponda alitiwa
mbaroni
Oktoba baada ya waandamanaji wa Kiislamu kutaharuki na kuchoma makanisa
matano
jijini Dare es Salaam.
Ghasia hizo zilizuka baada ya mvulana wa
Kikristu
kudaiwa kukojolea nakala ya Korani. Zaidi ya watu 120 walitiwa mbaroni
kufuatia
ghasia hizo, ambazo zilijenga uhasama mkubwa kati ya Waislamu na
Wakristu,
katika moja ya matukio mabaya zaidi ya kidini kuwahi kutokea katika
historia ya
Tanzania bara.
Kulikuwapo pia ghasia katika kisiwa cha
Zanzibar
wakati kiongozi mmoja wa dini ya Kiislamu, Shehe Farid Hadi Ahmed
alipotekwa
asubuhi ya Oktoba 16. Kanisa la Jimbo la Christ Church lilipo eneo la
Mji
Mkongwe kisiwani hapo lilishambuliwa na waamini wake kuondolewa haraka
ili
kuwanusuru.
Uganda haikupata matukio ya migogoro mikubwa ya
kidini
kama ilivyokuwa kwa Kenya na Tanzania.Lakini Mwinjilisi wa kanisa la
Pentekoste, ambaye aliwashawishi maelfu ya waumini ya Kiislamu kujiunga
na
Ukristu aliharibiwa uso wake wakati wa usiku wa Krismasi 2012, tukio
ambalo
lilileta hofu baina ya waumini wa dini hizo mbili pia.
Kwa nchi za Rwanda na Burundi hapakuripotiwa
matukio
yoyote yasiyo ya kawaida yaliyoleta mvurugano baina ya Waislamu na
Wakristu.