WANANCHI wa
kijiji cha Bugwema wilayani Butima mkoani Mara,wamemtuhumu mwenyekiti wa
kijiji
hicho kuiba Mahindi ya msaada ambayo yametolewa na serikali kwaajili ya
kukabiliana na njaa huku akiwalinda wezi wa mifugo katika kijiji hicho.
Wananchi hao
wametoa tuhuma hizo katika mkutano wa hadhara mbele ya mkuu wa mkoa wa
Mara Bw
John Tupa,ambayo amekuwa akiifanya katika vijiji mbalimbali kwaaji ya
kutafuta
njia sahihi ya kukabiliana na uhalifu yakiwemo mauaji ya kinyama katika
wilaya
hiyo.
Hata hivyo
mwenyekiti huyo wa Serikali ya kijiji hicho Bw Johanes Sando,amekiri
kuwepo kwa
tuhuma hizo ambapo amesema tayari zimefikishwa polisi ili kuona kama
zina
ukweli wowote huku mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo Bw Yahona Mirumbe
akivitaka
vyombo vya dola kuchukua hatua kwa kiongozi yoyote bila kujali cheo
chake ambaye
atabainika kujihusisha vitendo viovu vikiwemo wizi na mauaji.
Kwa upande
wake mkuu huyo wa mkoa wa Mara John Tupa,akizungumza katika mkutano huo
wa
hadhara ametoa wiki moja kwa viongozi na watu wote wanajihusisha katika
mtandao
wa wizi wa mifugo kujisalimisha wenyewe mara moja kwa mkuu wa polisi
wilaya kabla
ya jeshi la polisi kuwamata na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.
