KIZIMBANI KWA KOSA LA KUKUTWA NA NYARA ZA SERIKALI

MKAZI mmoja wa kijiji cha Mariwanda wilayani Bunda mkoani Mara Bw Weshi Phares Mhuku  amefikishwa katika mahakama ya wilaya hiyo kwa kukabiliwa na mashitaka mawili likiwemo la kukutwa na nyara za serikali kinyume cha sheria za uhifadhi wa wanyamapori.

Imedaiwa na mwendesha mashtaka wa idara ya wanyamapori Bw James Litereko mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo Bi Safina Semfukwe kuwa mbali na shitaka hilo pia mshtakiwa ambaye ni mkulima na mkazi wa
kijiji hicho anakabiliwa na shtaka la kutotoa taarifa za kumiliki nyara hizo za serikali.

Akifafanua mwendesha mashitaka huyo amesema mnamo Januari 15 mwaka huu majira ya saa nne na nusu asubuhi katika kijiji hicho cha Mariwanda askari wa wanyama pori  walimkamata Bw Weshi akiwa amepakia mbavu za pundamilia kwenye pikipiki yenye namba T 863 CDN ambazo amesema zinaashiria kuuwawa kwa mnyama huyo mmoja aliye na thamani ya shilingi milioni 1,920,000.

Amesema kwa kumiliki nyara hizo bila kutoa taarifa mshtakiwa anaingia moja kwa moja katika shitaka la pili la kutotoa taarifa kwa mamlaka husika kuwa anamiliki nyara kama inavyoainishwa na sheria namba 5 ya mwaka 2009 ya uhifadhi wa wanyamapori.

Mshtakiwa hakutakiwa kujibu chochote maana kesi yake ni ya uhujumu uchumi na amepelekwa rumande hadi  Januari 31 mwaka huu kesi yake itakapotajwa tena.

Wakati huo huo Bi Amina Maduhu mkazi wa kijiji cha Mariwanda afikishwa katika mahakama hiyo kwa kutuhumiwa kukutwa na vipande vinne vya nyama ya pundamilia vinavyoashiriwa kuuwawa kwa pundamilia mmoja mwenye thamani ya shilingi 1,920,000 bila kutoa taarifa kwa mamlaka husika.

Kwa mujibu wa mwendesha mashitaka huyo wa idara ya wanyamapori ameiambia mahakama kuwa mshtakiwa alikamatwa Januari 15 mwaka huu huko kijiji kwake majira ya saa nne na nusu ambapo ameiomba mahakama hiyo iiahirishe kesi hiyo kwani bado upelelezi bado
unaendelea  ambapo.
 
Kesi hiyo itatajwa tena januari 31 mwaka huu ambapo mshitakiwa huyo amerudishwa rumande baada ya mwendesha mashitaka huyo kuiambia kuwa kosa hilo ni la kuhuhumu uchumi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo