Mstahiki
Meya Jerry Silaa akipunga mkono kwa wanafunzi wa shule ya sekondari
Azania waliojipanga mstari kumlaki kwa furaha huku akiwa ameambatana na
Mkuu wa Shule hiyo Bw. Bernard Ngoze na Makamu Mkuu wa Shule hiyo Bi.
Elizabeth Ngoda (kulia).
Baadhi ya Wanafunzi wa
Shule ya Sekondari ya Azania wakiwa wamejipanga kumpokea mgeni rasmi
katika mahafali ya kidato cha Sita ya shule hiyo Mstahiki Meya wa
Manispaa ya Ilala Jerry Silaa yaliyofanyika leo jijini Dar.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya wa
Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akibadilishana mawazo na baadhi ya
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Azania ambapo na yeye pia alikuwa ni
miongoni mwa baadhi ya viongozi waliosoma shule hapo baada ya kuwasili
kwenye hafla mahafali ya wanafunzi wa kidato cha sita.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya
Jerry Silaa akisaini daftari la wageni la Shule ya Sekindari Azania
katika sherehe za mahafali ya Kidato cha sita shuleni hapo.
Mkuu wa shule ya Sekondari
Azania Bw. Bernard Ngoze akizungumza na mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry
Silaa na kumwelezea changamoto mbali mbali zinazoikabili shule hiyo. Wa
kwanza kulia ni Makamu Mkuu wa Shule hiyo Bi. Elizabeth Ngoda na Makamu
wa pili shuleni hapo Mwl. Joram Nkya.
Kutoka kushoto ni Mgeni
maalum aliyewahi kusoma shuleni hapo Bw. Ali Said Mwema, Mjumbe wa Bodi
ya Shule hiyo Bi. Hilda Luhanga na Msaidizi wa Meya Jerry Silaa Bw.
Anthony William wakimsikiliza mkuu wa shule ya sekondari Azania (hayupo
pichani) wakati akiongea na Mgeni rasmi.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya
Jerry Silaa akiongozwa na Makamu Mkuu wa Shule ya Azania Bi. Elizabeth
Ngoda kutazama baadhi ya picha zinazoonesha hali ya utunzaji wa
mazingira tangu awali mpaka sasa ambapo kwa kiasi kikubwa shule hiyo
imeweza kuboresha na kutoa elimu ya mazingira kwa wanafunzi wa shule
hiyo. Mstahiki Meya amepongeza juhudi zao na kuwataka shule nyingi za
jijini zilizochini ya manispaa ya Ilala kuiga mfano wa shule ya Azania
katika kutunza Mazingira.
Baadhi ya picha zikionesha
harakati za utunzaji wa Mazingira wa Shule ya Azania unaosimamiwa na
Mkuu wa Shule hiyo Bw. Bernard Ngoze ambaye naye alikuwa miongoni mwa
wanafunzi waliosoma shule hiyo.
Vijana wa Skauti wa shule ya
Sekondari Azania wakitoa heshima kwa mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry
Silaa alipowasili eneo maalum palipofanyika sherehe za mahafali ya
kidato cha Sita.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya wa
Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akisalimiana na kuwapongeza baadhi ya
wanafunzi wa kidato cha Sita wa Shule ya Sekondari Azania.
Mstahiki Meya Jerry Silaa
akipokea heshima kutoka kwa vijana wa skauti wa shule hiyo.
Kiongozi wa gwaride la
skauti la Azania akisalimiana na mgeni rasmi Meya Jerry Silaa.
Baadhi ya Wanafunzi wa
kidato cha sita wa shule ya Azania wakiimba wimbo wa Taifa baada ya
mgeni kuwasili.
Skauti wa shule ya Azania
wakiupa heshima wimbo wa Taifa.
Meza kuu ikiimbia wimbo wa
taifa.
Baadhi ya Wazazi na walezi
waliohudhuria hafla ya watoto wao.
Vijana wa Skauti wakionesha
manjonjo yao mbele ya mgeni rasmi kwenye mahafali hayo.
Binti Pekee wa kikundi cha
Skauti cha Azania sekondari aliyeshangaza wengi kwa kutembea na kamba
huku akijiamini vilivyo wakati wa sherehe za mahafali hayo.