Mpango
huu wa kusomesha watoto wa mkulima unaojulikana kama “Zabibu na shule
kwanza” ulizinduliwa rasmi mnamo tarehe 01 Julai
2011 Bungeni Dodoma na Spika wa bunge la Tanzania, mama Anna
Makinda.
Lengo
kuu la mradi huu ni kuhakikisha familia za wakulima walio kwenye mkataba
na TDL
wanafaidika na kazi za wazazi wao kwa kusaidia watoto wa familia hizo
kwenda
shule, kupunguza idadi kubwa ya watoto wanaoshindwa kuendelea na elimu
ya
sekondari kutokana na kukosa pesa za kulipia ada na mahitaji muhimu ya
shule kutoka kwa wazazi ama walezi wao ambao ni wakulima wa zao la
zabibu.
TDL
itakuwa imewapunguzia mzigo mkubwa na kuwapa wakulima hawa muda muafaka
wa
kujitatiti zaidi katika shughuli za kilimo cha zabibu ili kuziwezesha
familia zao kujikimu vizuri kimaisha.
Mradi
huu ulianza na watoto kumi (10), na mwaka jana tukaongeza watoto
ishirini (20) na
ni matarajio kuwa mwaka huu idadi ya watoto watakaopewa ufadhili itakuwa
wanafunzi ishirini (20), hivyo kufikisha idadi ya wanafunzi
wanaosomeshwa na
mpango huu kuwa wanafunzi hamsini (50).
TDL
kama kampuni tunaamini kuwa, uwekezaji kwenye elimu na pia kumsomesha
mtoto ni kukuza uchumi wa nchi yetu.