| Wanachama wa CCM tawi la chuo cha Mkwawa wakiwa na mabango mkatika mapokezi ya mangula leo |
| Umati wa wana CCM waliofika uwanja wa Mwembetogwa kumsikiliza Mangula |
| Makamu mwenyekiti wa CCM bara Philip mangula katikati akiwa na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu na mwenyekiti wa CCM wilaya ya Iringa mjini Abed Kiponza kulia |
MAPOKEZI makubwa ambayo ameyapata makamu mwenyekiti wa chama cha
mapinduzi (CCM)
Tanzania bara Philip Mangulla yametishia uhai wa chama cha
Demokrasia na maendeleo (Chadema) jimbo la Iringa mjini .
Huku
wanafunzi wa chuo kikuu kishiriki cha elimu Mkwawa wakimpokea
Mangula kwa mabango yenye jumbe mbali mbali ukiwemo wa kumpongeza
Mangula kwa kuteuliwa na ule unaolalamikia utaratibu mbovu wa
ucheleweshaji wa mikopo kwa wanafunzi hao wa vyuo vikuu pamoja na
kuitaka CCM
kukomesha vitendo vya rushwa ndani na nje ya chama.
Katika
historia ya CCM jimbo la Iringa na mkoa wa Iringa haijapata kutokea
mapokezi ya kishindo kama hayo baada ya umati mkubwa wa wananchi
kujitokeza kumpokea Mangula huku maeneo mbali mbali ya mji wa Iringa
yakipambwa kwa bendera za CCM mithiri ya makao makuu ya CCM Dodoma
wakati wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho.
Wakizungumzia
juu ya mapokezi hayo ya kishindo kwa Mangula baadhi ya wananchi
wameonyesha kutofautiana juu ya mapokezi hayo huku baadhi yao wakidai
kuwa maandalizi ya mapokezi hayo yamefanywa na Jesca Msambatavangu
ambae ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa ambae ni mwanamke wa
kwanza kuongoza chama hicho toka nchi ilipopata uhuru wake mwaka
1961 huku wengine wakidai kuwa ni matokeo ya kukubalika kwa
sekritaeliti mpya ya CCM akiwemo katibu mkuu wa CCM na mwenyekiti na
makamu wake bara na visiwani.
Katibu
wa umoja wa vijana wa CCM mkoa wa Iringa Rhoda George alisema kuwa
wananchi wa jimbo la Iringa mjini wamejitokeza kwa wingi katika
mapokezi hayo kutokana na utekelezaji mzuri wa Ilani ya CCM unaofanywa
na madiwani wake pamoja na wabunge wa CCM mkoa wa Iringa.
Hata
hivyo
alisema kuwa mapokezi
hayo makubwa kwa wananchi wa jimbo la Iringa mjini ni ishara nzuri
ya ushindi wa CCM katika uchaguzi wa serikali za mitaa pamoja na
uchaguzi mkuu mwaka 2015 katika jimbo hilo.
Kwa
upande wake Brown Payovela alisema kuwa wakazi wa mkoa wa Iringa
wameonyesha matumaini makubwa kwa Mangula na kuwa upo uwezekano mkubwa
wa CCM kuendelea kushinda kwa kishindo katika chaguzi
zake zijazo.
Baadhi
ya wananchi mashabiki wa vyama vya upinzani mjini Iringa walisema
kuwa CCM imetumia mbinu ya kunyong'onyeza nguvu ya vyama vya upinzani
katika jimbo hilo la Iringa mjini hasa chama cha Chadema ambacho
mbunge wake ni mchungaji Peter Msigwa .
Hivyo
walisema kuwa iwapo mbunge wa jimbo hilo Mchungaji Msigwa hatafanya
kazi zinazoonekana uwezekano wa kuambulia kura mwaka 2015 unaweza
kuwa mdogo japo walisema kuwa katika uchaguzi mkuu mwaka 2015
upinzani bado utategemea huruma za wana CCM kuendelea kumchagua mbunge
huyo ila iwapo CCM itafanya mchezo mchafu katika utaratibu wa kumpata
mgombea wa ubunge jimbo hilo.
Alisema
Damas Kalinga mkazi wa Kihesa ambaye alijitambulisha kuwa ni shabiki
wa Chadema kuwa hadi sasa ndani ya CCM jimbo la Iringa mjini tayari
wagombea wameanza kuwachanganya wananchi kwa kila mmoja kuonyesha
kuitaka nafasi ya ubunge na kuwataka viongozi wa CCM kuwa makini
zaidi.
Miongoni
mwa wabunge
waliojitokeza katika mapokezi hayo ni pamoja na mbunge wa viti
maalum mkoa wa Iringa Ritta kabati , mbunge wa jimbo la kalenga na
waziri wa fedha Dr Wiliam Mgimwa,makada wa CCM pamoja na wakuu wa
wilaya za Iringa , Kilolo na Mufindi wakiongozwa na mkuu wa mkoa wa
Iringa Dr Christine Ishengoma.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jasca Msambatavangu
akimkaribisha Mangula katika uwanja
huo wa Mwembetogwa kwa
ajili ya kuwahotubia mamia ya wananchi waliofika katika uwanja
huo alisema kuwa CCM itaendelea kueleza utekelezaji wa Ilani ya
uchaguzi kwa wananchi wake na kuwa tayari baadhi ya kata zimeanza
kutoa utekelezaji wa ilani hiyo kwa wananchi.
Msambatavangu
aliwapongeza wanachama wa vyama vya upinzani ambao wameanza kurudi
CCM na kuwa kurejea kwa wanachama hao wa vyama
vya upinzani ndani ya CCM
ni kutokana na utekelezaji mzuri wa ilani yake kwa wananchi na
uendeshaji wa CCM ndani ya CCM bila kunadi sera za matusi na ubaguzi .