Kwa mara ya kwanza juzi
january 10 2013 ndio zilitangazwa habari za msanii Mh Temba kuibiwa
vitu vya gari lake kwa mara ya tano, amekua na magari tofauti tofauti
ambapo kwa mara tano ameibiwa vitu mbalimbali ambapo baadae amekua
akilazimika kununua vitu vilevile vya kwake.
Hizi picha amezituma
Exclusive kwa millardayo.com na kusema huyu jamaa anatuhumiwa kuwa
mwizi hodari wa power window, vioo na vifaa vingine vya magari
mbalimbali ambapo alipohojiwa na polisi amesema yeye huwa ananunua tu
vifaa vya magari lakini hausiki kufanya wizi.
Wanaofanya wizi ni
wengine ndio wanamletea na yeye anafanya kazi ya kumpigia simu mwenye
mali ili aje avinunue vifaa vilivyoibiwa kwenye gari lake, sasa
kilichofanya Mh Temba amkamate ni pale alipopigiwa simu na huyu huyu
jamaa na kudai kwamba anavyo vifaa vilivyoibwa kwenye gari lake.
Hii
ndio Verosa ambayo waliiba vifaa ambavyo baadae Temba alikuja kuvinunua
kwa laki nane, na ni vifaa vilevile vilivyoibwa kwenye gari lake.
Kumbe huyu jamaa ndio
yule yule aliwahi kumpigia simu Temba wakati alipoibiwa tena vifaa vya
gari november 2012 na kumuuzia vifaa vilevile kwa shilingi laki nane
huku Temba akiitoa hiyo pesa akiwa anajua kabisa vifaa anavyonunua ni
vilevile, wakati huu Temba bado alikua ameisave namba yake kwa hiyo
akashtukia mchezo kwamba jamaa ndio wanamchezea hivyo akajipanga na
kwenda kumkamata.
Mtuhumiwa alipofikishwa
polisi akajitetea kwamba yeye hausiki na wizi, yeye anafanya udalali wa
kununua na kuuza hivyo vifaa tu na wala vitu vingine vinavyoibwa kwenye
magari kama Camera na Laptop huwa hausiki navyo na wala havinunui.
Polisi wanamjua kabisa na
namba yake wanayo kwa sababu jamaa amekua na kesi hizo mara nyingi sana
hapo kituoni, mara ya mwisho ambapo wengi wanaoibiwa vifaa huwa
anawaambia watume pesa kupitia line yake ya simu ya mkononi alafu
wakishatuma ndio mtu anatumwa kwenda kuvipeleka hivyo vifaa, kama
alivyofanya kwa Mh Temba mara ya mwisho na alitaka kufanya hivyo hata
wakati huu.
Mh Temba amerudishiwa
vifaa vyake alivyoibiwa wakati huu na mtuhumiwa ameachiwa, sio kwa
dhamana ila wamechukua tu alama zake za vidole wakamwambia arudi
jumatatu, Temba nae kaambiwa arudi jumatatu.
source:millardayo.com