Barabara ya Matamba - Nungu ambayo imetengenezwa kwa nguvu za wananchi
MC wa sherehe za mapinduzi akionesha wananchi kitita cha fedha zilizotolewa na CCM kuwaunga mkono wananchi hao kwa kujenga barabara hiyo
mwenyekiti wa CCM wilaya ya Makete Francis Chaula akizungumza na wananchi hao
Chama cha mapinduzi (CCM)
wilayani Makete kimewataka wananchi wa Makete kutodanganywa na kuyumbishwa na
mtu yeyote pindi wanaposhiriki katika shughuli za maendeleo katika wilaya yao
Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa
CCM wilaya ya Makete Bw. Francis Chaula wakati akitoa salamu za chama chake
katika maadhimisho ya miaka 49 ya mapinduzi ya Zanzibar yaliyoadhimishwa kiwilaya katika
kijiji cha Nungu kata ya Matamba
Amesema chama chake kimefarijika
kuona wananchi waliyochangia nguvu zao katika kuchimba na kutengeneza barabara
ya kutoka Matamba hadi Nungu, kwani hapo awali barabara hiyo haikuwepo na
badala yake ilikuwa ni njia ya waenda kwa miguu, na kusema jambo hilo linafaa kuigwa na
maeneo mengine wilayani hapo
Katika kuunga mkono jambo hilo mwenyekiti huyo alitoa fedha taslimu 50,000/= kama mchango wake wa kuunga mkono wananchi hao
kutengeneza barabara hiyo huku wadau mbalimbali walioambatana naye katika
maadhimisho hayo wakimuunga mkono kwa kumchangia mwenyekiti huyo na fedha hizo
kufikia Tsh. 130,000/= fedha ambazo zilikabidhiwa kwa mtendaji wa kijiji hicho
na kukatiwa risiti papo hapo
“Ndugu zangu hakuna mtu
asiyependa maendeleo na kitendo mlichokifanya wana nungu mimi kama mwenyekiti
wa CCM, tumefarijika sana na ndio maana mmeona wenzangu walivyoniunga mkono na
kuchanga 130,000/= ni kwa kuwa watu wanakipenda chama cha mapinduzi nawaombeni
fanyeni maendeleo achaneni na propaganda na hao wengine wanaokuja kuwadanganya
hapa” alisema
Hatua iliyobakia hivi sasa kwenye
barabara hiyo ni uwekaji wa kifusi ili isiteleze na iendelee kutumika kwa muda
mrefu na fedha hizo zilizochangwa moja ya kazi zake ni kusaidia uwekaji wa
kifusi