Na
Mwandishi Wetu
MWANAMITINDO
wa kimataifa wa Tanzania, Flaviana Matata ameendelea kung’ara kimataifa
baaada
ya kushinda tuzo ya Nigeria’s Next Super model na kuwa mwanamitindo bora
barani
Afrika wa mwaka 2012 (Africa’s Most Outstanding Model 2012).
Tuzo
hiyo utolewa kwa wanamitindo ambao bado wanailetea sifa Afrika kimataifa
na
Flaviana amekuwa katika chati ya juu. Mwaka jana Desemba, Flaviana
alishinda tuzo nyingine ya uwanamintindo bora kutoka kwa diaspora ya
Waafrika.
Flaviana
kwa ambaye kwa sasa anaishi na kufanya kazi ya uanamitindo New York
nchini Marekani kupitia shirika la Wilhelmina Models, mpaka sasa ameweza
kuitangaza Tanzania kimataifa kutokana na umahiri wake katika maonyesho
ya
mavazi.

Tangu
ashinde taji la Miss Universe Tanzania mwaka 2007, Flaviana amekuwa
aking’ara
katika kona zote za dunia na hasa baada ya kumaliza katika nafasi ya
sita
katika mashindano ya kimataifa ya Miss Universe, huku Tanzania
ikishiriki kwa
mara ya kwanza.
Ameweza
kushiriki katika maonyesho ya mavaz mengi Ulaya na Amerika huku akitoa
misaada
mingi kwa Watanzania wenzake ambao wamekuwa na ndoto ya kufika mbali
katika
fani hiyo.
Kwa
sasa Flaviana anaendesha taasisi yake, Flaviana Matata Foundation ambayo
inasomesha watoto wa kike 16 na mwaka jana alitoa msaada wa vifaa vya
kuokoa
maisha kama sehemu ya kumbukumbu ya kuzama kwa meli ya MV Bukoba huku
ikiwa
kumbukumbu ya kifo cha mama yake mzazi katika ajali hiyo ya mwaka 1996.
Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya Compass Communication Tanzania Limited, Maria
Sarungi
Tsehai alisema kuwa wamejisikia faraja sana kwa kumvumbua mwanamitindo
huyo
ambaye kwa sasa anashika chati ya juu Tanzania na nje ya nchi.
Maria
alisema kuwa Flaviana amedhihirisha ubora wake na mpaka sasa amepitiliza
kiwango cha kuitangaza Tanzania nje ya mipaka yake, ndoto ambayo alikuwa
nayo
muda mrefu.