Serikali
ya nchi za Hongkong na China zipo katika hatua za awali ilikufanya
makubaliano
ya kufanyabiashara ya nyama kutoka nchini Tanzania kupitia Kampuni ya
ranchi ya
taifa NARCO.
Afisa masoko wa kampuni ya NARCO Immanuel
Mzava amesema nchi hizo za Hongkong na China zinahitaji tani 75 za nyama
ya
ng’ombe ambazo zitakuwa zikiuzwa kupitia TMC katika kipindi cha mwezi
mmoja
ujao.
Amesema
kutokana ukubwa wa soko hilo NARCO inafanya mazungumzo na TMC kuangalia
uwezekano wa kuboresha baadhi ya vitendea kazi na mfumo wa upozeshaji
ili
kuweza kumudu ukubwa wa soko hilo.
Amesema
soko hilo pia litahitaji vifaa kama pembe, kwato, maini, ngozi na utumbo
ambao utasafirishwa
katika matunzo maalumu ikiwa ni sehemu ya oda ya soko hilo.
Hata hivyo
ndugu Mzava amewataka wadau mbali mbali ufugaji ng’ombe kutoa
ushirikiano wa
kupeleka ng’ombe ili kutosheleza soko hilo la nyama ikiwa ni pamoja na
mazungumzo yanaendelea kupata wakala atakayeuza Kongwa beef Dodoma mjini
ili
kuongeza mauzo ya ndani.
Ametaja
masoko mengine la ndani kuwa ni pamoja na nchi za Zambia ambalo tayari
wameanza
kupelekewa nyama ya ng’ombe 1000 wamechinjwa kupitia SAAFI na kuuzwa nje
ya
nchi na Zambia.
Aidha
akizungumia soko la ndani amesema NARCO amejipanga kufungua kituo cha
mauzo
Morogoro nanenane haraka iwezekanavyo ili kuongeza mauzo ndani ikiwa ni
pamoja
na kufungua bucha Mwenge, Mikocheni na Mbezi Beach.
