skip to main |
skip to sidebar
DIWANI AFUMANIWA UGONI IRINGA ACHEZEA KIPIGO.. SHUHUDIA
Katika
hali isiyo kuwa ya kawaida diwani mmoja wa chama cha siasa jina
laka na chama chake limewekwa kapuni kwa sasa amefumaniwa
akivunja amri ya sita na mke wa mtu usiku wa leo na kuchezea
kichapo.
Diwani
huyo mpenda ngono anadaiwa kufumaniwa akiwa katika nyumba ya mpiga
kura wake huyo katika kata moja ya wilaya ya Iringa Vijijini na
ni diwani anayetokea katika wilaya ya Iringa mkoa wa Iringa na ni
diwani mtanashati kweli kweli.
Mashuhuda
wa tukio hilo wameudokeza mtandao huu kuwa kutokana na fumanizi hilo la
mwaka wapiga kura wake wanaoishi jirani na nyumba hiyo ambayo
mheshimiwa alifunaniwa waliizunguka nyumba hiyo na kuanza kumshikisha
adabu mheshimiwa huyo.
Baada
ya mheshimiwa huyo kuchezea kipigo kutoka kwa njema lenye mke
huyo pamoja na wananchi alilazimika kutoka mbio na kukimbilia porini
kabla ya kwenda kupatiwa matibabu katika moja kati ya zahanati
mbili zilizopo katika eneo hilo ikiwemo ya Misheni na ile ya Kijiji.
Iwapo
wataka kujua zaidi juu ya tukio hili endelea kufuatilia mtandao
huu unapofanya jitihada za kumtafuta diwani huyo
Pichani ni moja kati ya picha ya fumanizi ambayo inafanana
na fumanizi hili la diwani japo hainamahusiano na tukio hili na www.francisgodwin.blogspot.com
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi