Wakati Serikali ikihamasisha usafi wa
mazingira katika maeneo yote nchini, Chama cha Wananchi CUF mkoani Tanga
kimetoa tamko la kupinga zoezi hilo lililopangwa kufanyika kila
Jumamosi kwa madai kwamba wanachama wake watakuwa kwenye shughuli za
kimaendeleo.
Akitoa tamko hilo kwenye mkutano wa hadhara Diwani wa
Msambweni, RADHID JUMBE amesema, suala hilo ni la kisiasa na kwamba
limepangwa ili kukujenga Chama cha Mapinduzi CCM kisiasa.
Mkuu wa Mkoa
wa Tanga CHIKU GALAWA amewataka wananchi mkoani humo kushiriki zoezi la
Usafi kila Jumamosi kufuatia kushuka kwa utekelezaji wa zoezi hilo kama
ilivyopangwa hapo awali.
Hatua hiyo ya Viongozi wa CUF kutangaza mgomo
wa kushiriki zoezi la ufanyaji wa usafi katika maeneo yao limedaiwa
kuchangiwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga kutowashirikisha madiwani
wa chama hicho katika kuutekeleza mpango huo.