Mtu
mmoja amefariki Dunia Mkoani Dodoma katika tukio la ajali ya gari
kumgonga mtembea kwa miguu na kusababisha kifo.
Tukio
hilo limetokea tarehe 14/01/2013 majira ya saa 09:30
alasiri katika kijiji cha Kelema Wilaya ya Chemba barabara
ya DODOMA -KONDOA baada ya gari lenye namba za usajili T.
769 BNP aina ya Scania Bus mali ya Kampuni
ya Champion likendeshwa na dereva aliyefahamika kwa jina
la George s/o Maiko Kwayu likitokea Dodoma kuelekea Kondoa
kumgonga mtembea kwa miguu na kumsababishia kifo chake
papo hapo.
Marehemu
ametambuliwa kuwa ni Mohamed s/o Hassan mwenye umri wa Miaka(110)
Mrangi ambaye ni mkazi wa kijiji cha Kalamba kuu Kelema wilayani Chemba.
Uchunguzi
wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa Dereva kwa
kutokuwa mwangalifu kwa watumiaji wengine wa barabara kwani alikuwa
katika mwendo wa kasi katika eneo lenye makazi ya watu
kinyume na sheria za usalama barabarani zinavyoelekeza.
Madereva
wanatakiwa kujua na kuzingatia ni mwendo gani watumie katika maeneo
tofauti wanayopita, kama Kifungu namba 51, kifungu kidogo cha 8 (a) cha
sheria ya Usalama barabarani ya Mwaka 1973 iliyofanyiwa
marekebisho mwaka 2002 sura ya 168 ambayo inatamka bayana kwamba mtu
yeyote anayetumia chombo cha moto barabarani haruhusiwi kuendesha chombo
hicho zaidi ya spidi 50 kwenye makazi ya watu.
Napenda
kutoa wito kwa madereva wote kuzingatia sheria, taratibu na kanuni za
usalama Barabarani ili kuepusha ajali zisizo za lazima, ambazo
hulipunguzia taifa nguvu kazi.
Mtuhumiwa
anashikiliwa na Jeshi la Polisi na atafikishwa mahakamani pindi
uchunguzi utakapokamilika.
DAVID MISIME-
ACP
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA DODOMA
