NA FRANCIS GODWIN
BAADA ya kukamilisha zoezi zima la uanzishaji wa chama cha kuweka na kukopa cha klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC VIKOBA) sasa klabu hiyo ya wanahabari mkoa wa Iringa imekuja na wazo wa kumiliki kituo cha radio kitakachojulikana kama Radio IPC FM.
BAADA ya kukamilisha zoezi zima la uanzishaji wa chama cha kuweka na kukopa cha klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC VIKOBA) sasa klabu hiyo ya wanahabari mkoa wa Iringa imekuja na wazo wa kumiliki kituo cha radio kitakachojulikana kama Radio IPC FM.
Mwenyekiti mpya wa IPC Frank Leonard ameyasema hayo leo wakati akifanya mahojiano na vyombo mbali mbali ukiwemo mtanddao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com na Zenji FM ya Zanzibar kuhusiana na mkakati wa klabu hiyo baada ya kukamilisha zoezi la uanzishwaji wa IPC VIKOBA na kuziba nafasi za viongozi ndani ya klabu hiyo.
Leonard amesema kuwa kutokana na nguvu inayoendelea kuonekana ndani ya IPC kabla ya kifo cha aliyekuwa mwenyekiti wa IPC Daud Mwangosi na sasa ni wazi kuwa mkakati huo utafanikiwa na utakuwa ni ukombozi mkubwa kwa wanahabari mkoa wa Iringa.
Hata hivyo alisema wakati akiwa katibu mtendaji wa IPC na Mwangosi akiwa mwenyekiti katika moja kati ya vikao vya kamati ya utendaji suala hilo la kuanzisha kituo cha radio lilijadiliwa kwa kina japo utekelezaji wake haukuanza ila sasa IPC imepania kulisimamia wazo hilo ambalo lilitolewa chini ya uongozi wa Marehemu Mwangosi na kuungwa mkono na wanachama wote.
Alisema kuwa sehemu kubwa ya wanachama wa IPC ni wanahabari ambao wanafanya kazi katika vyombo mbali mbali ila baadhi yao ni waandishi wa kujitegemea hivyo iwapo IPC itaanzisha kituo hicho cha radio kitakuwa ni ukombozi mkubwa kwa wanahabari wanaofanya kazi zao kwa kujitegemea kwa kusimamia radio hiyo.
Pia alisema kuwa moja kati ya mipango ya kuwa na radio hiyo ni kuweza kutoa mfano mwema kwa vituo vya radio Fm hapa nchini ambazo baadhi zinaendeshwa kinyume na maadili ya utangazaji na hivyo kituo hicho cha radio IPC FM kitasaidia kuonyesha mfano wa namna gani radio FM zinaweza kuendeshwa kwa maslahi ya jamii zaidi badala ya kuendeshwa kinyume na maadili.
katika hatu nyingine Leonard amesema kuwa IPC kwa kushirikiana na baraza la habari Tanzania (MCT ) imeanzisha kamati ya usuluhishi kwa ajili ya kutoa nafasi ya wananachi ambao wanaripotiwa vibaya katika vyombo vya habari kuweza kufikisha malalamiko yao kwa kamati hiyo na wahusika kuhojiwa .
Alisema kamati hiyo itafanya kazi yake kwa wanahabari wote bila kujali kuwa ni mwanachama wa IPC ama si mwanachama na kuwataka wananchi ambao wataona wameandikwa ama kuripotiwa vibaya na chombo chochote cha habari kufika IPC ili kukutana na kamati hiyo kabla ya kukimbilia mahakamani.
Kamati hiyo ya usuluhishi inaundwa na wajumbe nane ikiongozwa na wakili maarufu mkoani Iringa mheshimiwa Dismas Mmbando ambae ni mwenyekiti wa kamati hiyo
