Jeshi la Polisi linaonekana kufanya kazi zaidi kwa mazoea kuliko kuzingatia mafunzo wanayopewa, pichani ni askari polisi aliyejeruhiwa na wenzake baada ya kupigwa marungu kwa kutomjua kama nayeye ni askari hadi alipopiga kelele ‘mtaniua mimi mwenzenu’ ndipo wakamuachia.
Kilichofuata baada ya askari huyo kuachiliwa na
wenzake alimalizia hasira zake zote kwa wanafunzi hao kwa kutembeza
kipigo
(mkong’oto) mkali kwa wanafunzi Chuo Cha IFM waliojaribu kutaka
kulazimisha
jeshi la polisi kufanya mkutano mbele ya kituo cha Polisi Kigamboni
badala ya
kwenye viwanja vya mpira eneo la Machava Kigamboni bila kujali kuwa
wanafunzi
hao walikuwa wakikabiliana na moshi nzito wa mabomu ya machozi lakini
pia
walisha kuwa chini ya ulinzi mkali na hakukuwa na sababu yeyote ya
kuwapiga
hivyo.
Mbali na askari huyo kulikuwepo
na askari wengine wawili akiwemo mmoja wakike nao pia waliambulia kipigo hicho.
Fuatilia picha za Askari huyo na matukio aliyofanya .
Fuatilia picha za Askari huyo na matukio aliyofanya .
Picha hii
inakuonesha kwa karibu namna
rungu lilivyompasua Askari huyu, hapa utapata picha kama huyu askari
aliyepigwa kidogo tu baadaye akaachiwa ameumia hivi je wale waliopata
mkong'oto wapo kwenye hali gani.
Hapa anazuia damu
sehemu aliyopigwa isindelee kuvuja kwa kutumia kitambaa.
Baada
ya kupata nafuu anakuja kumalizia hasira zake kwa wanafunzi kwa
kumkamata mmoja na kumpa kipigo cha nguvu hadi askari wenzake
walivyopiga kelele ndipo alimwachilia mwanafunzi huyo.
Hakuishia
hapo aliwafuata pale walipoamrishwa kukaa akawa anamchomoa anaemtaka na
kumpa kipigo vile alivyojiskia
ili amalizie hasira zake.
Kumbuka kipigo hicho
kinafanyika mbele ya kituo cha polisi huku kukiwa na ulinzi mkali
umeimarishwa.
Alichagua kama
maembe au mpira na kuchezea alivyotaka!
