KLABU ya waandishi wa
habari mkoa wa Iringa (IPC) imekamilisha kuziba mapengo ya uongozi
yaliyokuwepo ndani ya IPC kufuatia kifo cha aliyekuwa mwenyekiti
wake marehemu Daud Mwangosi aliyeuwawa tarehe 2/9/2012 Nyololo katika
vurugu za polisi na Chadema kwa kumchangua Frank Leonard kuwa
mwenyekiti mpya wa klabu hiyo huku Francis Godwin akiwa katibu mkuu
wa IPC.
Mbali ya kuziba nafasi
hiyo ya mwenyekiti kwa Leonard aliyekuwa katibu mtendaji kuamua
kugombea uenyekiti na Godwi aliyekuwa katibu msaidizi kugombea ukatibu
mkuu pia wajumbe wa mkutano huo wame mchagua Janeth Matondo kushika
nafasi ya mweka hazima mkuu wa IPC nafasi iliyokuwa wazi baada ya
aliyekuwa mwekahazina Vicky Macha aliyefariki mwezi mmoja baada ya
kifo cha Mwangosi .
katika mkutano huo maalum wa uchaguzi huo uliofanyika leo katika Hotel ya M.R mjini Iringa msimamizi mkuu wa uchaguzi huo Frederick Siwale aliwataja waliochaguliwa kuwa ni pamoja na aliyekuwa katibu mtendaji wa IPC Frank Leonard aliyepata kura 17 kati ya kura 18 zilizopigwa katika nafasi hiyo ya uenyekiti iliyokuwa ikigombewa na mwanachama Zulfa Shomari aliyetangaza kujitoa na kuomba wajumbe kumchagua Leonard kutokana na utendaji wake mzuri .

Wakati makamu mwenyekiti
amepita bila kupingwa Jackson Manga aliyepata kura zote 18 za
wajumbe wa mkutano huo ambao jumla ya wanachama hai wa IPC ni 24
na 18 ndio waliofika katika mkutano huo nafasi ya katibu mtendaji
wa IPC imechukuliwa na aliyekuwa naibu katibu mkuu wa IPC Francis Godwin
aliyepata kura za ndio 16 huku kura 2 zikimkataa .
Wengine waliochaguliwa ni pamoja na mweka hazina mkuu wa IPC Janeth Matondo aliyechukua nafasi ya marehemu Vicky Macha kwa kupata kura zote za ndio 18 pamoja na mweka hazina msaidizi Suleiman Boki aliyepata kura zote 18 .
Wajumbe watatu wa kamati ya utendaji waliochaguliwa ni Hapy Matanji aliyepata kura (18) Swiga Mwaisumbe (18 ) na Selina Ilunga(17).