MKAZI
mmoja wa Kijiji cha Mnazi kilichopo Kata ya Ulumi wilayani Sumbawanga
mkoani Rukwa, Prisca Dickson mwenye umri wa miaka 17, anashikiliwa na
polisi kwa tuhuma ya kutupa mtoto wake chooni mara baada ya kujifungua,
kwa hofu ya kuachwa na mchumba wake.
Taarifa
zinasema kuwa, mtoto huyo wa siku moja ametupwa katika choo cha jirani,
akiwa ameviringishwa katika kipande cha kanga. Kamanda
wa Polisi mkoani Rukwa, Jacob Mwaruanda amesema kuwa, Prisca amemtupa
mtoto huyo mara baada ya kujifungua, na kusababisha kifo chake kutokana
na kukosa hewa ambapo mwili wa kichanga hicho umegunduliwa na wanafunzi
wa Shule ya Msingi Mnazi ambao walipita asubuhi katika nyumba hiyo ya
jirani na mmoja wao aliingia chooni kujisaidia na kukuta maiti hiyo
ikielea kisha alitoa taarifa.
Kamanda Mwaruanda
amesema kuwa, baada ya uchunguzi imebainika kuwa Prisca ndiye aliyefanya
kitendo hicho. Ameongeza kuwa, binti huyo amedai
kuwa imemlazimu kufanya hivyo kwa kuwa, ujauzito aliokuwa nao ni wa
mwanaume mwingine. Mtuhumiwa anatarajiwa kufikishwa
mahakamani mara baada ya kukamilika kwa uchunguzi wa tukio hilo.