| Meneja Mkuu wa Kampuni ya Green Waste Pro, Elizabeth Scheepers akishiriki kufanya usafi |
| Usafi ukiendelea kufanyika katika eneo hilo |
| Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa (kulia), alikuwa ni miongoni mwa viongozi waliojitokeza kufanya usafi baada ya kuzinduliwa kwa kampeni hiyo. |
| Lundo la vifuu vya madafu vikiwa kando ya ufukwe wa Bahari ya Hindi katika eneo hilo na kuharibu kabisa mandhari ya ufukwe huo, vifuu hivyo viliondolewa katika kampeni hiyo. |
Joshua Palfreman ambaye alijitolea
kufanya usafi katika uzinduzi wa kampeni hiyo akiokota takataka katika
uzinduzi wa kampeni hiyo.
Na Dotto Mwaibale
MEYA wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa leo amezindua kampeni ya usafi katika jiji la Dar es Salaam hasa maeneo ya Kati kati ya jiji.
Kampeni hizo zimefunguliwa na Meya huyo na kuhudhuriwa na wadau wengine mbalimbali kutoka sekta binafsi, wananchi na viongozi wa kampuni ya Green Waste pro.
Silaa alitoa mwito kwa wakazi wa Manispaa ya Ilala kujenga tabia ya kushiriki katika usafi wa jiji kuanzia kwenye kata na kuwa uzinduzi wa leo umehusisha Kata tatu ambazo ni Kata ya Kivukoni, Mchafukoge pamoja na Kata ya Kisutu.
"Kwa kuanzia tumeanza na kata hizi katika Manispaa ya Ilala lakini baadae zitahusishwa na Manispaa nyingine ili kuliweka jiji katika hali ya usafi.