MNYIKA KUFANYA MKUTANO MKUBWA WA HADHARA MANZESE JIJINI DAR LEO

Mbunge John Mnyika

IKIWA ni siku moja tangu Mbunge wa Jimbo la Ubungo kupitia CHADEMA, John Mnyika ashinde kesi yake iliyokuwa ikipinga ubunge wake, leo atafanya ziara kubwa katika Jimbo la Ubungo ndani ya Kata ya MANZESE!
Ziara itanza majira ya saa 4 asubuhi ofisi ya kata (Kilimani), na hapo atafungua misingi maeneo ya mitaa ifuatayo; Kilimani, Chakula bora, Mvuleni, Midizini, Mwembeni na Mnazi mmoja.

Vile vile kuanzia saa 10 alasiri atafanya Mkutano Mkubwa wa Hadhara eneo la Mtaa wa Mnazi Mmoja (nyuma ya jengo la Msangi karibu na eneo la kwa Mfuga Mbwa). Hoja: Ufisadi mkubwa TANESCO, URAFIKI, Maoni Katiba Mpya!

Short URL: http://www.thehabari.com/?p=25816


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo