Na Riziki Manfred
Mkuu
wa mkoa wa Njombe Kepteni mstaafu Asery Msangi amefanya ziara ya kushtukiza
katika shamba la ngano lililoko kijiji cha Ludodolelo kata ya Mang’oto wilaya
ya Makete baada ya kupata malalamiko kutoka kwa wananchi wanaozunguka shamba hilo
Mkuu
huyo wa mkoa amefanya ziara hiyo hii leo akiwa ameongozana na mkuu wa wilaya ya
Makete Bi Josephine Matiro pamoja na viongozi wengine ili kujionea uendeshwaji
wa shamba hilo
ambalo baadhi ya wananchi wamekuwa wakilalamikia uendeshwaji wake
Shamba
hilo linalomilikiwa na kampuni ya SELUE COMPANY LIMITED limelalamikiwa na
wakazi wa eneo hilo kwa madai kume kuwa na umwangaji wa dawa ya kuuwa magugu
shambani wakati wauandaaji wa mashamba hayo na dawa hiyo inayosadikika kuwa ni
sumu imekuwa ikisambaa katika mashamba ya wakazi hao na kuharibu mazao ikiwemo miti pamoja na uchafuzi
wa vyanzo vya maji
Wameeleza
kuwa dawa hiyo imekuwa ikitiririka hadi kwenye chanzo cha maji kinachopeleka
maji kwenye kijiji chao na Njombe mjini jambo ambalo ni hatari kwa watumiaji wa
huduma hiyo.
Aidha
kabla ya kufanya ukaguzi katika shamba hilo mkuu wa mkoa aliongea na mmoja wa
wasimamizi wa shamba hilo ambaye alikiri kutumia dawa hiyo ambapo amesema wamekuwa waangalifu
pindi wanapo mwaga dawa hiyo kwani wanatambua umuhimu wa afya za binadamu na
wamekuwa wakishirikisha wataalamu wakati wa umwagaji dawa hiyo na kukanusha
malalamiko ya wananchi kuwa si kweli.
Baada
ya kupokea taarifa hiyo mkuu wa mkoa pamoja na msafara wake walielekea kukagua
shamba hilo ambapo hawakuona mazao wala miti iliyoathiriwa na dawa hilo jambo
ambalo liliibua maswali mengi kwa mkuu wa mkoa na kutaka kujua uhusiano uliopo
kati ya mwekezaji huyo na wananchi wanaozunguka eneo hilo.
Katika
hatua nyingine mkuu wa mkoa amemtaka mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya Makete
kuwa karibu na wawekezaji waliopo wilayani mwake kwani kufanya hivyo kutasaidia kudhibiti mapato ya halmashauri ili kufikia
malengo yanayokusudiwa na serikali