Na Charles Charles
“KUZUNGUKA
huku na huko kwa CCM ni kutuiga sisi.
Tumeanza muda mrefu baada tu ya uchaguzi
mkuu
wa mwaka 2010”, ndivyo anavyosema Katibu Mkuu wa
Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema),
Dk. Willibrod Slaa.
Anaongeza
kwamba “Chadema ni mwalimu” huku Chama
Cha Mapinduzi (CCM) kikiwa mwanafunzi
anayefuata
nyayo kwa mambo yanayofanywa na chama chake hicho.
Alikuwa
akizungumza na gazeti moja la kila siku
nchini kufuatia ziara iliyofanywa hivi
karibuni na Katibu
Mkuu wa CCM, Kanali Abdulrahman Kinana katika
mikoa minne ya
Arusha, Geita, Mtwara na Rukwa.
Siku
chache baadaye, yeye mwenyewe alifanya ziara
katika majimbo matatu ya Temeke,
Kigamboni na
Kinondoni jijini Dar es
Salaam na kukumbana na hali
ngumu kuliko wakati wote
uliopita.
Tatizo
hilo
liliambatana na ‘kudoda’ kwa harambee
ya kuchangia kile kinachoitwa kuwa ni
Vuguvugu
la Mabadiliko (M4C) iliyofanyika jijini Mwanza, na
kukitia chama hicho
hasara ya shilingi milioni tisa.
Wakati
hayo yakiendelea, Katibu wa Halmashauri Kuu
ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na
Uenezi, Nape Nnauye
aliibua tuhuma kwa Dk. Slaa kuwa pamoja na
kuwashambulia sana
viongozi wenzake wilayani Temeke
akisema ni mamluki wa CCM, yeye mwenyewe ana
kadi
ya chama hicho kinachotawala, jambo alilokiri
ni kweli na ataendelea kuitunza katika
maisha yake yote.
Tayari
hali hiyo imeibua mtafaruku katika chama
chake ambapo kuna wanachama, viongozi
na wafuasi
wake hivi sasa hawana tena imani naye na kuanza
kumtilia wasiwasi
kwa kusema inawezekana pia ndiye