Na Riziki Manfred, MAKETE
Jeshi la polisi wilayani Makete linamshikilia mwanamke mmoja
mkazi wa Malembuli wilayani hapa kwa kosa la kumzika akiwa hai mwanaye wa
kumzaa mwenyewe na kutorokakea jijini Mbeya.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo mkuu wa polisi wilaya
Makete Peter Kaiza amemtaja mwanamke huyo kuwa ni Bi Fatuma Sanga mkazi wa
kijiji cha Malembuli ambapo mnamo desemba 14 mwaka huu Bi Sanga alimzika mtoto huyo akiwa hai
mwenye umri wa mwezi mmoja.
Bwana Kaiza amesema Bi Sanga baada ya kutenda tukio hilo alitorokea jijini
Mbeya na polisi baada ya kupata tarifa
kutoka kwa raia wema walilazimika kumfuata na kufanikiwa kumkamata
Aidha inadaiwa kuwa Bi Sanga alimzika mtoto huyo nje kidogo
ya eneo analoishi ambapo alidaiwa kuwa alimzika mtoto huyo baada ya kufariki
dunia lakini taarifa kutoka kwa mashuhuda zinasema huenda mtoto huyo aliuawa
kabla ya kuzikwa ama alizikwa akiwa hai
Hata hivyo jeshi la polisi likuwa likimshikilia Bi Sanga
pamoja na mumewe ambaye kwa sasa ameachiwa baada ya maelezo ya Bi Sanga kuwa mumewe
hahusiki na wala hakujua chochote kuhusu tukio hilo
Bi Sanga anatarajiwa kufikishwa katika mahakama ya wilaya ya
Makete baada ya uchunguzi wa awali
kukamilika
Hilo
ni tukio la pili kutokea katika kata hiyo baada ya tukio lingine lilitokea
mwaka 2009 katika kijiji cha Makangalawe ambapo mwanamke mmoja alimtupa mtoto
wa siku tatu katika mto Masalala