Mwenyekiti wa baraza la wazee wa CCM wilaya ya Makete Mzee Amos Sukunala Nkwama wakati akiongea na waandishi wa habari
Serikali imeshauriwa kusimamia
kwa karibu masilahi ya watumishi wakiwemo waalimu, madaktari na wengine ili
huduma ziendelee kutolewa kma zilivyotarajiwa kwa wananchi
Rai hiyo imetolewa na baraza la
wazee wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Makete kupitia kwa mwenyekiti wake
Mzee Amosi Sukunala Nkwama wakati akizungumza na waandhshi wa habari kwenye
ofisi za chama hicho wilaya
Pamoja na hayo baraza hilo limeomba sheria ya matibabu bure kwa wazee ifanye
kazi kama ilivyopitishwa ili kuwalinda wazee
wanapopata maradhi wakati wowote
“Unajua watu wanatusahau sisi
wazee na kutudharau kana kwamba hatuwezi kufanya chochote, tukienda hospitalini
tunatozwa fedha, wakati hatuna uwezo wa kufanya kazi, lakini ikumbukwe sisi
wazee ndio tuliohangaikia huduma hizi tangu zinaanzishwa wakati sisi tukiwa
vijana kama wao” alisema Nkwama
Naye Katibu wa CCM wilaya ya
Makete Miraji Mtaturu ambaye pia ni katibu wa baraza la wazee ndiye aliyeyasoma
maazimio hayo mbele ya waandishi wa habari ambapo yapo maazimio sita
Mbali na hayo ya awali mengine ni
kumpongeza mwenyekiti wa Taifa Dkt Jakaya Kikwete kwa kura za kishindo
alizopata na kupewa ridhaa ya kuongoza chama kwa miaka kitano ijayo, Kuupongeza
mkutano mkuu wa taifa ulivyoendeshwa kwa kuchagua viongozi mahari, wachapakazi
na wazalendo kwa chama na chi kwa ujumla, kuupongeza mkutano mkuu kwa namna
ulivyofanyika kwa kuonesha dira ya mafanikio katika kuisimamia serikali na
kutekeleza wajibu wake kwa wananchi pamoja na kuendelea kuunga mkono juhudi za
mwenyekiti wa CCM Taifa kupiga vita ufisadi, uzembe na vurugu za kisiasa
zinazopelekea uvunjifu wa amani