
Mifuko ya Saruji 24 iliyoharibika

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Mlaguzi, Antony Msagala (CCM) akitoa Tamko la Viongozi wake kusema Uongo na kumdharilisha juu ya Ubadhirifu wa Zahanati 2
---
Bryceson Mathias, Mlaguzi Mvomero
ALIYEKUWA
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Mlaguzi, Antony Damiani Msagala
(Gambus) (60) amesema, licha ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kumdhaLilisha
na kumfedhehesha, bado viongozi wake wamejiumbua kwa kusema uongo
kuhusu ubadhirifu wa Ujenzi wa Zahanati na kuacha Mifuko ya Saruji 24 ya
thamani ya sh. 384,000/-Kuganda.
Msagala
alisema hayo akisherehekea Krismas 25.12 ikiwa siku chache baada ya
wananchi wa Mlaguzi kuupiga Chini Uongozi wa watu 17 wa Halmashauri ya
Serikali ya CCM akiwemo yeye na Katibu wake Daudi Kikoti aliyefariki
ghafla ambapo Idadi kubwa ya wakazi walijiunga na Chama Demokrasia na
Maendeleo,
Akizungumza na
Mwandishi aliyekuwa akikagua zahanati iliyotolewa taarifa kwenye
Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero kwamba iko kwenye hatua ya Lenta wakati
iko kwenye Msingi wa Magoti (picha zimeambatanishwa - tunazo),
Mwenyekiti huyo alisema,
“Nilishangaa
Uongozi wa Kata ya Sungaji kutaka niwape Mihutasari ya maamuzi
yaliyofanywa na vikao kuhusu mapato na matumizi ya fedha zilizotengwa
kwa ajili ya Ujenzi wa Zahanati hiyo, na kinachonisikitisha ni taarifa
ya Uongo iliyotolewa ati Ujenzi uko kwenye Lenta wakati iko kwenye
Msingi.
Kwenye Kikao halali tuliidhinisha zichukuliwe Benki Mil. 410,000/- sasa kikao kilichoidhinisha Mil. 4.8/- zilizochakachuliwa
sijui Mwenyekiti wake alikuwa nani na muhutasari aliupitisha nani mie
sihusiki,…lakini hao wanotaka niutoe ule halali tuliopitisha ili
wachakachue siwapi labda waniue”.alisema Msagala.
Naye Katibu
Mwenezi wa CCM kijijini hapo Method Malishali Clemence Pichani alisema
ameamua kujiuzulu Uenezi wa Chama kwa madai hawezi kueneza Uongo maana
ni aibu, na akadai kuna mifuko 24 ya saruji iliyoganda ya Laki 384,000/-
ambayo ni hasara.
Aidha Viongozi
mbalimbali akiwemo Kiongozi wa Dini ya Romani Katoliki (RC) Katekista
Emmanuel Gabriel Chambo, Aliyekuwa Mgombea wa Kata ya Sungaji (CHADEMA)
Jairos Msigwa, na Diwani Mstaafu wa Kata ya Sungaji Waziri Chamwenye
(CCM), walilalamikia Mil. 4.8/- Kati ya Mil.36 za Mradi huo kutumika
vibaya, ambapo Katekista Chambo alidai, anasikitishwa anasikitishwa na
waumini wanaose Uongo kwa kuwa
hakuna Mchanga au Mawe yaliyonunuliwa ila wananchi walisomaba akiwamo yeye.
hakuna Mchanga au Mawe yaliyonunuliwa ila wananchi walisomaba akiwamo yeye.