WAKILI WA LORD EYEZ AFUNGUKA KUHUSIANA NA KESI INAYOMKABILI MSANII HUYO


Msanii wa Bongo Fleva kutoka A town city almaarufu kama Lord eyez ambaye siku za hivi karibuni alikabiliwa na kesi ya kuiba vifaa vya gari sasa

Latest Info ni kwamba msanii huyu pamoja na Wakili wake waliamua kuweka wazi juu ya kesi inayomuanda hivi sasa.Wakili huyu anayekwenda kwa jina la Peter Kibatala alisema kwamba kesi hii imefanya mpaka Lord Eyez kuonekana kwamba yeye ndiyo mhusika wa kuiba vifaa hivyo lakini sasa hivi wanaachia kwanza Mahakama ndiyo itakayo chukua uamuzi sahihi kuhusiana na kesi hiyo.
 
Lakini hapo hapo tuliweza kusikia ujumbe kutoka kwa weusi walizungumza na kusema kwamba tukio kama ili limewaathiri pale wanapokutana na watu mbalimbali na kusikia story za watu kusema kwamba wote watakuwa wanahusika katka kesi hiyo wakati ni story ambazo sio za kweli.
 
Baada ya hapo tuliweza pia kusikia ujumbe kutoka kwa Lord Eyez mwenyewe  aliweza kuzungumza kusema kwamba mahakama ndiyo itaamua kuchukua sheria kwamba alihusika au ajahusika katika tukio kama hilo la kuiba vifaa vya gari,ambayo kesi hiyo inatarajia kusomwa Mahakama ya Mwanzo siku ya tarehe 13,14 na 15 mwezi huu hapa jijini Dar es Salaam lakini pia alimalizia kwa kusema japokuwa  kwa sasa hivi yupo kitaani huku akisikilizia  Mahakama imeamuaje kwa hiyo anachotaka kukifanya ni anataka kudondosha ngoma yake mpya kali ambayo anataka kufanya suprise kwa mashabiki wake katika industries hii ya muziki wa Bongo Fleva.
                                                                     Lord Eyez
                                                                      Nikki wa Pili
                                                                         G nako
                                                        Lord Eyez akiwa na wakili wake

                                                                        Weusi!!!!!!!!!
Picha na stori kwa hisani ya djfetty.blogspot.com


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo