RAIS JAKAYA KIKWETE ASHIRIKI MAZIKO YA ASKOFU BALINA HUKO SHINYANGA

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho akitia saini kitabu cha maombolezo ya kifo cha Mhashamu Baba Askofu Aloysius Balina wa Jimbo Katoliki la Shinyanga baada ya kuwasili kwenye Kanisa la Mama wa Huruma katika Parokia ya Ngokolo mjini Shinyanga kushiriki mazishi ya Askofu huyo leo, Jumamosi, Novemba 10, 2012.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Mhashamu Baba Askofu Aloysious Balina wa Jimbo Katoliki la Shinyanga wakati wa mazishi wa Askofu huyo kwenye Kanisa la Mama wa Huruma, Ngokolo, mjini Shinyanga leo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kwenye kaburi la Askofu Aloysius Balina wakati wa mazishi ya Askofu huyo leo kwenye Kanisa la Mama wa Huruma, mjini Shinyanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la maua kwenye kaburi la Askofu Aloysius Balina wa Jimbo Katoliki la Shinyanga wakati wa mazishi ya Askofu huyo kwenye Kanisa la Mama wa Huruma, Ngokolo, Shinyanga leo. Picha na mdau Fred Maro-Ikulu


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo