Imeelezwa kuwa maandalizi ya ujenzi wa vyoo bora katika shule ya msingi Ivalalila kata ya Iwawa wilayani Makete tayari umeanza
Akizungumza na mwanahabari wetu ofisini kwake Afisa mtendaji wa kijiji cha Ivalalila Bw. Fidelis Sanga amesema kuwa mpaka sasa wameshachimba uwanja, kukusanya mawe, tofali pamoja na kukusanya kokoto
Amesema ujenzi huo wa vyoo bora katika shule hiyo umefadhiliwa na shirika la AMREF kwa kushirikiana na wananchi wa kijiji hicho kutokana na vyoo vinavyotumika hivi sasa shuleni hapo kukosa ubora
Bw. Sanga amesema hakuna changamoto yeyote iliyojitokeza wakati wa maandalizi ya vifaa vya ujenzi huo kutokana na wananchi wa kijiji hicho kujitoa kwa wingi kushiriki kwenye mradi huo kwa kushirikiana kuandaa vifa hivyo na kuvisogeza hadi kwenye eneo la ujenzi
Mtendaji huyo ametoa wito kwa wananchi kuendelea kuchangia asilimia 20 inayotakiwa katika utekelezaji wa mradi huo, huku akiwaomba pia wafadhili hao kuwasilisha msaada wao kwa wakati ili ujenzi huo ukamilike kama unavyotarajiwa
Na Hadija Sanga