Na Ibrahim Yassin,
IMEELEZWA kitendo cha kukithiri kwa vitendo vya uvuvi haramu vinavyo fanywa na wavuvi katika forodha mbali mbali katika ziwa nyasa wilayani Kyela Mbeya ni moja ya sababu inayoifanya Halmashauri ya wilaya hiyo kuigia kwenye kashfa ya kupuuza agizo la waziri mkuu Mizengo Pinda alilotoa siku za nyuma akiiagiza wizara ya maendeleo ya mifugo na uvuvi kuhusu usalimishaji wa zana haramu za uvuvi,
Wakizungumza na waandishi wa habari akiwemo mwandishi wa mtandao huu Ibrahim Yassin waliofanya ziara ya kushtukiza kwenye forodha hizo mara baada ya kupata taarifa ya kuwepo kwa vitendo vya uvuvi haramu,baadhi ya wakazi wanaoishi pembezoni mwa ziwa hilo walidai kuwa wavuvi hao wamekuwa wakitumia nyavu zilizowekwa vyandarua katikati na kuvua dagaa waliokatazwa kisheria huku wakiharibu mazalia ya samaki,
Walidai kuwa pamoja na jitihada za maafisa uvuvi kufanya doria mara kwa mara ya kuwasaka wavuvi hao lakini bado tatizo linaendelea kuwa sugu,kutokana na uchache wa maafisa hao ukilinganisha na uwingi wa wavuvi na idadi nyingi za forodha zilizopo pembezoni mwa ziwa hilo,
Afisa uvuvi wa wilaya ya Kyela, Yusuph Baraka alipoulizwa na wanahabari kuhusu kukithiri kwa vitendo vya uvuvi haramu kwenye ziwa hilo,alikiri kuwepo kwa uvuvi huo na kudai kuwa wamefanya jitihada nyingi za kuwadhibiti wavuvi hao lakini zoezi linaonekana kuwa gumu kutokana na uchache wao na pia katika msaka walioufanya mwishoni mwa mwezi huu wamefanikiwa kukamata nyavu 10 zilizowekwa vyandarua katikati na nyavu 50 za ngerwa zilizokuwa na macho madogo,
Awali waziri mkuu Mizengo Pinda aliiandikia barua wizara hiyo yenye kumbukumbu na pm/p/569 142 ya tarehe 18/01/2010,iliyohusu kusalimisha zana haramu za uvuvi na kuitaka sheria ya uvuvi ya mwaka 2003 na kanuni zake za mwaka 2009 zinazoelekeza matumizi ya nyavu za kuvulia dagaa,
Barua hiyo iliandika kuwa ,nyavu zinazotakiwa kuvulia dagaa ni zile zenye ukubbwa wa macho yasiyopungua milimita 8 kwenye maji baridi,na milimita 10 kwenye maji chumvi,hatua hiyo ilichukuliwa ili kuhakikisha wingi wa dagaa unaogezeka kwenye maji hayo na utafiti utakapoonyesha mabadiliko ya rasilimali hizo kanuni hizo zitabadilika,
Kutokana na agizo hilo la maandishi la waziri mkuu,Halmashauri ya wilaya ya Kyela imeonekana wazi wazi kuwa imekaidi agizo hilo kutokana na wavuvi wanaotumia ziwa nyasa kuendelea kuvua uvuvi haramu huku wakiharibu mazalia ya samaki kwa kutumia nyavu zilizowekwa vyandarau katikati,
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela ,Clement Kasongo alisema kuwa ni kweli tatizo hilo lipo lakini vijana wake waejitahidi kufanya doria za mara kwa mara zilizo fanikisha kukamata nyavu 60 zilizo kuwa zikitumika kuvulia samaki kinyume na taratibu za zilizo wekwa na kuongezwa kuwa operesheni hiyo ni endelevu,
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Gabriel Kipija,kwa upande wake alidhibitisha kuwepo kwa vitendo hivyo na kudai kuwa halmashaur yake kupitia idara ya uvuvi inakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwapo ya upungufu wa watumishi wa idara hiyo,ukosefu wa boti speed kwa ajili ya kufanyia doria majini,na pia watazipeleka changamoto hizo wizara husika ili kuzipatia majibu changamoto hizo.
Unaweza kuwasiliana na mwandishi huyo kwa simu 0653369996,0767269996.
|
SERA MPYA YA ELIMU YAZINDULIWA
1 hour ago