UAMUZI WA SPIKA KUHUSU TUHUMA KWAMBA BAADHI YA WABUNGE NA
WAJUMBE WA KAMATI YA NISHATI NA MADINI WALIJIHUSISHA NA VITENDO VYA RUSHWA KATIKA KUTEKELEZA KAZI ZAO ZA KIBUNGE
WAJUMBE WA KAMATI YA NISHATI NA MADINI WALIJIHUSISHA NA VITENDO VYA RUSHWA KATIKA KUTEKELEZA KAZI ZAO ZA KIBUNGE
[Chini ya Kanuni ya 5(1) na 72(1) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la 2007,na Kifungu cha 12(1), (2)na 25(c) cha Sheria ya Kinga, Madaraka na Haki zaBunge, Sura ya 296]
________________
SEHEMU YA KWANZA
________________
SEHEMU YA KWANZA
Maelezo ya Utangulizi
Waheshimiwa Wabunge, mtakumbuka kwamba, tarehe 27 na 28 Julai, 2012 wakati wa mjadala waHotuba ya Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini, baadhi ya Wabunge walitoa michango mbalimbali na kuibua tuhuma zilizotolewa pia kwa maandishi, kwa barua ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Bw. Eliakim C. Maswi, kwa Katibu wa Bunge kama ifuatavyo:-

Kwamba, baadhi ya Wabunge na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini walikuwa wanaenda Ofisini kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini kuomba rushwa ili waitetee Wizara hiyo inapowasilisha taarifa mbalimbali kwenye Kamati hiyo;
Kwamba, baadhi ya Wabunge na Wajumbe wa Kamati hiyo wana mgongano wa kimaslahi (conflict of interest) katika kutekeleza majukumu yao ya kibunge ya kuisimamia Wizara ya Nishati na Madini, kwa kufanya biashara na Shirika la Usambazi wa Umeme (TANESCO);
Kwamba, baadhi ya Wabunge wamekuwa wanajihusisha na vitendo vya
rushwa kwa kupokea fedha kutoka kwenye Makampuni ya mafuta, kwa lengo la kuyatetea Makampuni hayo kwa kupinga uamuzi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Bw. Eliakim C. Maswi wa kutoa Zabuni ya Ununuzi wa mafuta mazito ya kuendeshea mitambo ya IPTL kwa Kampuni ya PUMA Energy (T) Ltd;

Kwamba, kutokana na kupewa rushwa na baadhi ya Makampuni ya mafuta ili wayatetee, baadhi ya Wabunge walikuwa wanaendesha kampeni ya kukwamisha kupitishwa kwa Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini, kwa mwaka wa Fedha 2012/2013.
Wakati wa mjadala huo, Mheshimiwa Vita Rashid Mfaume Kawawa (MB.) alitoa hoja kwa mujibu wa Kanuni ya 5(1), 53(2) na 55(3) (f) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la 2007 kwamba, kwa kuzingatia kuwamichango mingi iliyotolewa na Wabunge wakati wa kuchangia Hotuba hiyo imewatuhumu baadhi ya Wabunge na Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini kujihusisha na vitendo vya rushwa, anaomba mambo yafutayo yafanyike:-
Kamati ya Bunge na Nishati na Madini ivunjwe; na Tuhuma za vitendo vya rushwa zilizotolewa zifanyiwe uchunguzi na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.
Baada ya Mheshimiwa Vita Rashid Mfaume Kawawa kuwasilisha hoja yake, Bunge lilipitisha Azimio kwamba, “Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ivunjwe; na pia kwamba, tuhuma za vitendo vya rushwa zilizotolewa zichunguzwe na Kamati Ndogoya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge na kumshauri Spika.”
Katika kutekeleza Azimio hilo la Bunge, niliivunja Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, kwa kutoa tamko la kufanya hivyo Bungeni, kwa mamlaka niliyonayo kwa mujibu wa Kanuni ya 113(3), ikisomwa pamoja na Kifungu cha 48(1) (a) cha Sheria ya Tafsiri za Sheria, Sura ya 1 [The Interpretation of Laws Act (Cap.1)].
Aidha, kwa kuzingatia kuwa kwa hali-asili yake, jambo hilo linahusu ‘haki za Bunge’ (Parliamentary privilege), nililipeleka kwenye Kamati Ndogo ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ili Kamati hiyo ilifanyie uchunguzi na kunishauri.
Kamati hiyo Ndogo ilipewa Hadidu ya Rejea moja tu, ambayo ni:“Kuchunguza na kumshauri Spika iwapo tuhuma kwabaadhi ya Wabunge na Wajumbe wa Kamati yaNishati na Madinikujihusisha na vitendo vya rushwa ni za kweli au hapana.”
Baada ya Kamati hiyo kukamilisha kazi yake, iliwasilisha taarifayake rasmi
kwangu ili kwa wakati muafaka,niweze kutoa Uamuzi wa Spika kuhusu suala hilo.
kwangu ili kwa wakati muafaka,niweze kutoa Uamuzi wa Spika kuhusu suala hilo.
Kwa kuzingatia kuwa suala hilo linahusu “haki za Bunge,” (parliamentary
privilege),napenda nitoemaelezo ya ufafanuzi kuhusu dhana hiyo kabla ya
kutoa Uamuzi wa Spika.
privilege),napenda nitoemaelezo ya ufafanuzi kuhusu dhana hiyo kabla ya
kutoa Uamuzi wa Spika.
Dhana ya Haki za Bunge (Parliamentary Privilege) na Madhumuni yake
Kwa ajili ya Uendeshaji bora wa shughuli zake, Bunge kwa mujibu wa Katiba na Sheria, limepewa kinga,madaraka na haki, fulani (immunities, powers and privileges) ambazo zinaliwezesha kutekeleza majukumu yake kwa niaba ya wananchi, kwa uhuru, uwazi na uwajibikaji, bila ya kuingiliwa au kutishwa na mtu au chombo chochote cha Dola.

Katika Kitabu chake kiitwacho “Treaties on the Law, Privileges, Proceedings and Usage of Parliament,1Erskine Mayametoa tafsiri ya ‘haki za Bunge’ kama ifuatavyo:
“Parliamentary privilege is the sum of the peculiar rights enjoyed by the House collectively… and by Members of the House individually, without which they could not discharge their functions”2
Kwa tafsiri, nukuu hiyo inaeleza kwamba, “maana ya haki za Bunge ni haki zote za kipekee za Bunge na za kila Mbunge binafsi kwa ujumla wake, ambazo bila kuwepo kwake, Bunge na Wabunge hawawezi kutekeleza majukumu yao.”
Mwandishi mwingine aitwae Hood Phillips3 ameeleza kwamba, kila Bunge
linatekeleza madaraka na haki ambazo zinachukuliwa kuwa ni muhimu kwa hadhi ya Bunge, na pia katika kuliwezesha Bunge kutekeleza majukumu yake.
linatekeleza madaraka na haki ambazo zinachukuliwa kuwa ni muhimu kwa hadhi ya Bunge, na pia katika kuliwezesha Bunge kutekeleza majukumu yake.
Kwa ajili ya ufasaha zaidi, maelezo ya Mwandishi huyo kwa lugha aliyoitumia yanasomeka kama ifuatavyo:-
Kwa taarifa zaidi bonyeza hapa www.thehabari.com/habari-tanzania/makinda-atoa-ripoti-ya-tuhuma-za-rushwa-kwa-wabunge-kamati-ya-nishati-na-madini