Na Ibrahim Yassin, Kyela
KUTOKANA vitendo vya rushwa vinavyodaiwa kukithiri kwenye hospitali za Kyela mkoani Mbeya vilivyodaiwa na diwani kata ya Ipinda Dr,Hunter Mwakifuna alipokuwa akichangia hoja ya kamati ya afya elimu na maji kwenye kikao cha baraza la madiwani akiwatuhumu wa watumishi wa idara ya afya kuomba rushwa kwa wagonjwa wanaotumia dawa za ARVs,watumishi wa idara hiyo wapata mshituko,
Dr,Hunter Mwakifuna ambaye pia ni mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi wilayani hapa alitoa shutuma hizo alipokuwa akichangia hoja ya kamati hiyo iliyowasilishwa na Tuhumaini Ambakisye kwenye kikao cha Baraza hilo lililofanyika juzi kwenye ukumbi wa Community Center,alisema tuhuma dhidi ya watumishi hao ni aibu na zinapaswa kukomeshwa,
Alisema kuwa kwa muda mrefu madiwani wamekuwa wakipokea malalamiko mengi kutoka kwa wagonjwa wanaotumia dawa za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi ARVskuwa baadhi ya wahudumu katika kitengo hicho kwenye hospitali hizo wanawaomba rushwa ili wawape huduma hiyo ingawa hakutoa ushahidi kuhusiana na tuhuma hizo,
Katika hatua nyingine madiwani hao pia walilalamikia kukosekana kwa jokofu la kuhifadhia maiti kwenye hospitali hizo na kuwa kitendo hicho hakiendani na ali halisi ya wilaya hiyo yenye wasomi wengi na watumishi wengi wa ngazi za juu akiwemo waziri,
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kyela Clement Kasongo alijibu tuhuma hizo kwa kuwataka madiwani hao wampelekee ushahidi wa kutosha dhidi ya tuhuma hizo za watumishi wanao daiwa kutomba rushwa kwa wagonjwa hao ili aunde tume ya kuchunguza tuhuma hizo,
Mwenyekiti wa Baraza la watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi (KONGA)wilayani Kyela mkoani mbeya,Julius Mwalubalile alipohojiwa na Tanzania daima kuhusiana na tuhuma hizo zinazohusu watu wake kuombwa rushwa na watumishi wa idara ya afya katika hospitali hizo pindi waendapo kuchukuwa dawa za ARVS,alikana kuwepo na tuhuma hizo,
Mwalubalile alidai kuwa yeye ni mwenyekiti wa watu hao hajawahi kuletewa taarifa zinazohusu watu wake kuombwa rushwa na kuwa kimsingi kama tuhuma hizo zingekuwepo taarifa zingekuja ofisini kwake kwa maandishi na yeye angezipeleka kwenye uongozi wa juu ili kupatwa ufumbuzi wa tatizo hilo,
“Mimi ni mwenyekiti wa baraza hilo hapa wilayani kama tatizo hilo lingekuwepo ningeletewa malalamiko ofisini,na pia idara ya afya wilayani hapa imeweka mpango wa kupeleka dawa za ARVs kwenye zahanati zilizopo vijijini ili watu wachukue dawa hizo kwenye vijiji vyao,lakini wagonjwa hao wanaacha kuchukua dawa huko wakiogopa kunyoshewa vidole, wanakimbilia hospitali ya wilaya kitu ambacho kinaleta msongamono mkubwa wakati wa zoezi la ugawaji wa dawa hizo”,alisema Mwalubalile,
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kyela Gabriel Kipija kwa upande wake alikana kuwepo kwa vitendo hivyo vya rushwa kwenye hospitali hizo na kudai kuwa kama vitendo hivyo vipo yeye kama mwenyekiti angeletewa taarifa,wanaodai kuwa vitendo hivyo vipo wamekurupuka hawajafanya uchunguzi wa kutosha,isipokuwa wanataka umaarufu wa kisiasa,
Kipija ameitaja changamoto inayoikabili idara hiyo kuwa ni jengo la kutolea dawa za ARVs kuwa ni dogo ukilinganisha na idadi kubwa ya wagonjwa wanaokuja kuchukuwa dawa hizo na kudai kuwa wapo kwenye mchakato wa kuongeza jingo ili ilikupanua wigo wa huduma hiyo itakayopunguza msongamano wa wagonjwa wanaofika hospitalini hapo kuchukua dawa.