Mtangazaji wa Kitulo FM Aldo Sanga akinywa maji hayo baada ya kiu kumbana
Mmiliki wa mtandao huu Edwin Moshi naye akikata kiu na maji hayo
Kwa asilimia kubwa vijiji ambavyo vipo mbali na makao makuu ya wilaya ya Makete vina changamoto ya kupata maji ya bomba, kama inavyoonesha hapa kuwa kijiji cha Uganga kata ya Luwumbu wilayani Makete sehemu nyingi wakazi wake hutumia maji ya mifereji ambayo sio salama sana kwa kunywa kama njia ya kuendeleza shughuli za majumbani ambazo ni kufua, kupikia, kunywa nk, pamoja na shughuli za kilimo.
Hapa ni miongoni mwa sehemu ambayo wakazi hao wamepatengeneza kwa bomba la mti aina ya muanzi ili waweze kukinga maji