Mbali na kutembelea miradi hiyo ambayo mradi wa maji wa visima virefu,zahanati ya Didia na Kituo cha Polisi Didia pia amezungumza na wananchi wa kijiji cha Chembeli kilichopo katika kata ya Didia.
Matiro alikuwa ameambatana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Shinyanga lakini pia watalaam mbalimbali kutoka halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo,Bakari Kasinyo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiangalia bomba la maji ya kisima kirefu katika kijiji cha Chembeli.Mradi upo katika kijiji cha Didia na Bukumbi lakini kijiji cha Chembeli kimesaidiwa mabomba mawili kwa ajili ya wananchi hata hivyo changamoto ni kwamba bomba linaloleta maji limekuwa likipasuka mara kwa mara hivyo kusababisha kero kwa wananchi
Hapa ni katika moja ya eneo ambapo bomba la maji limekuwa likipasuka na wananchi kulazimika kulifunga kwa mapira/kamba za kuvutika.Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisikiliza maelezo kwa Mhandisi wa maji wa halmashauri ya Shinyanga Vijijini Sylivester Mpemba (wa tano kulia)
Bomba likiwa limefungwa kwa mapira/kamba za kuvutika baada ya kupasuka hivi karibuni
Mhandisi wa maji wa halmashauri ya Shinyanga Vijijini Sylivester Mpemba akielezea namna inavyotokea bomba la maji lipasuke.Hata hivyo mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro alimuagiza kufuatilia na kuchukua hatua madhubuti kuhusu tatizo la bomba la maji kupasuka mara kwa mara katika kijiji cha Chembeli
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza na wananchi wa kijiji cha Chembeli ambapo aliwataka kutunza mradi wa maji uliopo katika kijiji hicho sambamba na kuwahamasisha kulima mazao yanayostahili ukame kama vile mtama,uwele badala ya kutegemea mahindi pekee ili kukabilina na njaa
Wakazi wa kijiji cha Chembeli wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
Mkazi wa kijiji cha Chembeli akielezea kero zilizopo katika kijiji hicho
Mkazi wa kijiji cha Chembeli Maria Tungu akielezea kero ya maji katika kijiji hicho ambapo wanawake wanalazimika kusafiri umbali mrefu kufuata huduma ya maji katika visima na mto unaounganisha kijiji hicho na kijiji jirani cha Buyubi
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akimsikiliza mkazi wa kijiji cha Chembeli wakati akielezea kero yake
Diwani wa kata ya Didia Luhende Masele akizungumza katika kijiji cha Chembeli
Katibu tawala wilaya ya Shinyanga,Boniface Chambi akizungumza katika kijiji cha Chembeli
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Vijijini Bakari Kasinyo
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwasili katika kitongoji cha Danduhu kijiji cha Didia ambapo mkazi wa eneo hilo Mashaka Mayala Komanya amejenga nyumba juu ya mradi wa maji
Nyumba iliyojengwa juu ya mradi wa maji
Diwani wa kata ya Didia Luhende Masele akimweleza mkuu wa wilaya hatua walizozichukua kutokana na mwananchi huyo kujenga nyumba juu ya mradi wa maji ya visima virefu uliopo katika kata hiyo ikiwa ni kukubaliana bomba linalopita katika nyumba hiyo lihamishiwe karibu na barabara kwani halipitishi maji kwa sasa.Masele alisema mwenye nyumba hiyo anadai mradi huo ulipitishwa hapo bila yeye kushirikishwa
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akimuagiza mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Vijijini kuhakikisha taratibu za vikao zinafuatwa kwa kuandika muhtasari wa makubaliano watakayoyafikia ili kupata muafaka kuhusu jengo hilo kujengwa juu ya mradi wa maji na kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Vijijini Bakari Kasinyo akimpa maelekezo afisa mtendaji wa kijiji cha Didia Shimba Waziri(wa pili kulia) kuhusu nyumba hiyo kujengwa juu ya mradi wa maji.
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog