Na Ezekiel Kamanga, Mbozi
Mchungaji wa Kanisa la Reedemed Gospel Church John Mgalah(38) lililopo Kijiji cha Namlonga, Kata ya Ruanda, Wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya, anadaiwa kumpa mimba muumini wake Mariam Mwakabata(18), Mkazi wa Kijiji cha Idibila Wilayani humo.
Tukio hili ni kufuatia muumini huyo kudai alipigiwa simu na mchungaji huyo mnamo Selida Mtafya mwenye watoto sita akiwa amekwenda wilaya ya Mbeya katika Hospitali ya Ifisi kupatiwa matibabu.
Mariam amedai kuwa aliwasili kijijini hapo akitokea Mji mdogo wa Tunduma, alipokuwa amekwenda kuwasalimu kaka zake majira ya saa 11 wakati mchungaji akishiriki harusi ya Bwana Mika Msolina iliyokuwa ikifungwa kanisani hilo.
Aidha binti huyo amedai kuwa mchungaji alimtaka kutangulia nyumbani kwake naye kuitikia wito wa mchungaji, ambapo aliwasili saa 3:00 usiku na mchungaji kuwasili majira ya saa 4:00 usiku na kumtaka binti aende nyumba ya nje na kisha kukubali na mara baada ya mchungaji kufika alianza kumtomasasehemu mbalimbali, hali ambayo ilimfanya binti huyo kupiga kelele na mchungaji kutoka nje.
Mchungaji alirejea mara ya pili ndani ndipo alipofanikiwa kumbaka na kumsababishia ujauzito sasa ni miezi mitatu.
Baada ya kupitia mwezi mmoja kupita Binti huyo alimpigia simu mchungaji na kumueleza hali halisi ambapo alimtaka binti huyo kuitoa mimba na kumpa shilingi 20,000, lakini Mariam alipokea pesa hizo lakini hakwenda kuitoa mimba hiyo.
Binti huyo alianza kuutaarifa uongozi wa kanisa kufuatia mimba hiyo hiyo ndopo mchungaji alianza na yeye kukamilisha mchungaji alianza naye kukamilisha kumpa ujauzito huo.
Kwa upande wake Mchungaji alikanusha kuhusika na tendo hilo na kwamba binti uyo ana nia ya kumchafua tu ingawa binti huyo kulala kwake siku hiyo ya harusi na kudai alikuwa na ugomvi wa na familia yake.
Hata hivyo Askofu wa Kanisa hilo, Tawi la Mlowo wilayani humo Anyimike Mwaitumile amekiri kupokea shauri hilo na kwamba wanafanya uchunguzi na pindi atakapobainika watamchukulia hatua za kinidhamu kwa mtumishi huyo na kwamba wachungaji wa kanisa hilo wanatakiwa kujiepusha na mabinti kwani wanaweza kuwatondosha katika imani.
Wakati huo huo Serikali ya Kitongoji kupitia Bwana Asaulile Mwakimwili amesema kuwa suala hilo lipo kwenye Ofisi yake na wameweza kukutana na pande zote mbili na Mchungaji kukanusha lakini suala hilo likiwa limefikishwa katika Ofisi ya serikali ya kijiji chini ya Mwenyekiti wa Kijiji Bwana Asavule Mwakimwile na Afisa Mtendaji wa kijiji Bwana Beck T Siwale na kudai kuwa wanachosubiri barua ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.