Siku chache baada ya msanii nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini Ommy Dimpoz kuibiwa vifaa kutoka gari yake, mtangazaji mahiri wa kipindi cha 'Kwa Raha Zetu' kinachorushwa na Clouds Fm ya jijini Gea Habib naye amekutana na dhahma hiyo baada ya wakora kuiba vifaa kutoga ndinga yake ya kisasa aina ya GX110.
Akizungumza na Blog hii mapema leo Gea amesema kuwa aliibiwa vitu hivyo mwishoni mwa wiki iliyopita maeneo ya Kigogo na siku moja iliyopita alipigiwa simu na watu wasiojulikna wakimtaka kutoa kiasi cha shilingi milioni moja na nusu ili aweze kuvipata tena vifaa hivyo.
"Nimepigiwa simu 'leo' huyo mtu kaniambia vifaa vyangu vyote vipo isipokuwa natakiwa nitoe shilingi Milioni1.5 kuvipata, hawa watu hawana hata aibu na inaelekea ni watu ambao wanatufahamu na wanajua kila mtangazaji anamiliki gari gani" alisema Gea.
Hata hivyo uchunguzi uliofanya na blog hii umebaini kuwepo kwa tetesi zinazoenezwa na kundi moja la vijana kuwa kuna mpango wa kuwaibia watangazaji wote maarufu vifaa kutoka magari yao ili kuwakomoa kutokana na namnaa walivyolizungumzia suala na kuibiwa kwa nyota wa Bongo fleva Ommy Dimpoz.