Rais huyo wa kwanza mweusi kuliongoza taifa kubwa zaidi duniani ametangazwa asubuhi ya leo kuwa mshindi katika mchuano mkali na wa aina yake.
Ilikuwa ni kama ndoto iliyozimika katika makao makuu ya kampeni ya Mitt Romney mjini Alabama wakati matokeo yakianza kumiminika hasa kutoka katika majimbo yenye maamuzi ambayo yote yalikuwa yanaelekea kwa rais Obama.
Wakati kimya kikitanda katika kambi ya Romney na wafuasi wake wakionekana kutoamini kilichotokea, jimboni Chicagohali ilikuwa ya nderemo na vifijo.
Wafuasi wa chama cha Democrats wakishangalia wakati matokeo yakiendelea kutolewa.
Mitt Romney ameshinda kura ya umma kwa asilimia 50 lakini mfumo wa Marekani unazingatia kura za majimbo kupata mshindi. Obama ameshinda licha ya rekodi mbaya ya uchumi na ukosefu mkubwa wa ajira. Hakuna raia aliyewahi kupata muhula wa pili tangu kumalizika kwa vita vikuu vya pili vya dunia, kukiwa na ukosefu wa ajira wa zaidi ya asilimia 7.2. Kiwango cha sasa ni asilimia 7.9.
Matokeo yalianza kwa kutangazwa ushindi wa Rais Obama katika jimbo la Vermont, yakifuatia majimbo ya Delaware, Maryland, Michigan, Pennyslivania, Wisconsin na New Hampshire . Kwa na mpinzani wake Mitt Romney alinyakua ushindi wa mikoa inayofahamika kuegemea upande wa chama chake cha Republican, ikiwa ni pamoja na Kentucky, Tennese, South Carolina, West Virginia na Indiana.
Romney agoma kukubali kushindwa
Kambi ya Romney ilikuwa imeahidi kutokubali kushindwa, wakipinga matokeo katika jimbo la Ohio, lakini wachambuzi waliashiria kuwa hayatoleta mabadiliko yoyote katika ushindi wa Obama
Obama ameweza pia kushinda New jersey. Itakumbukwa wakati wa kimbunga cha sandy alilitembelea jimbo hilo la kupongezwa na Gavana wa New Jersey ambaye ni kutoka chama cha Republican.
Mfuasi wa Romney Alicia Hayes akifarijiwa na mama yake baada ya taarifa kuwa mgombea wake ameshindwa.
Wakati suala la uchumi na ukosefu wa ajira limewavutia zaidi waliompigia kura Romney, masuala muhimu kwa wapiga kura wafuasi wa Obama ni pamoja na bima ya afya. Pia baadhi wanahisi kuwa hatua za kuurekebisha uchumi zimeanzaa kuzaa matunda. Waliompinga Romney wana wasiwasi kwamba huenda akawapendelea zaidi matajiri.
Sambamba na matokeo haya ya uchaguzi wa rais kuna uchaguzi katika maeneo 33 ya uchaguzi kuwania viti vya baraza la wawakilishi ambalo linadhibitiwa na Warepublican.
Inaelekea wademocrats watashindwa kufanikiwa kupata viti 25 ambavyo watahitaji kulirudisha baraza hilo kwenye mamlaka yao.