Halmashauri ya Manispaa ya Iringa
imekuwa ikishindwa kutekeleza baadhi ya mikakati ya mipango ya mji na
mipango
mingine ya maendeleo kutokana na uwepo wa vijiji saba, jambo linaloleta
mkanganyiko wa kiutendaji ndani ya Manispaa.
Akiwasilisha mapendekezo ya kufuta
vijiji katika Manispaa ya Iringa katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya
Mkoa wa
Iringa, Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa, Theresia Mahongo ameitaja
sababu kuu
ya Halmashauri kutaka kufutwa kwa vijiji hivyo kuwa ni Halmashauri ya
Manispaa
kupanua mipaka yake kama inavyoelekezwa
kwenye
fungu la 12 la ‘The Local Government (Urban Authorities) Act, 1982.
Amesema
kifungu cha 12 kijifungu (1) kinasema kwamba Waziri mwenye dhamana
anaweza
kutangaza kwenye Gazeti la Serikali kufuta kijiji ama kijiji cha ujamaa
kilichoingia kwenye mipaka ya eneo la Mji.
Akielezea hali halisi, Theresia
amesema kuwa Manispaa yake imekuwa ikipata matatizo ya kiutendaji katika
maeneo
ya vijiji husika na kusababisha baadhi ya mikakati ya mipango ya mji na
mipango
mingine kutokukamilika.
Ameyataja baadhi ya matatizo hayo kuwa ni
kufanana kwa
baadhi ya kazi za Halmashauri ya Manispaa na Halmashauri ya kijiji jambo
linalosababisha kupingana katika suala la kiutendaji na utoaji wa
maamuzi.
Vilevile, amesema mvutano katika kutekeleza mipango thabiti na madhubuti
ya
Halmashauri ya Manispaa katika eneo lake la kiutawala na kusababisha
baadhi ya
mipango kutokutekelezwa katika maeneo ya kiutawala ya kijiji.
Matatizo mengine Mkurugenzi wa
Manispaa ya Iringa ameyataja kuwa ni suala la Ardhi ambalo limekuwa ni
kikwazo
kikubwa katika Mpango wa Mji na vijiji, kwa kuzingatia Sheria
zinazolinda
vijiji, vijiji vimepewa ruhusa ya kuuza, kuzuia na kuendeleza Ardhi ya
kijiji
bila ya kuingiliwa na mamlaka yoyote.
Ameongeza kuwa Sheria ya Ardhi ya
vijiji
Na. 5 ya mwaka 1999 kifungu cha 8(1) kinaeleza kuwa Halmashauri ya
kijiji kwa
kuzingatia masharti ya Sheria hii itawajibika kusimamia Ardhi yote ya
kijiji.
Amesema kwa tafsiri ya kifungu hicho, Halmashauri ya Manispaa ambayo
ndiyo
inayoshughulika na Mpango wa Mji, haitakuwa na mamlaka kuingia na
kutekeleza
Mpango wowote wa Mji katika eneo la kijiji.
Theresia ameyataja manufaa
yatakayopatikana baada ya kufutwa vijiji kuwa ni pamoja na Mipango ya
Matumizi
bora ya Ardhi inayojumuisha huduma muhimu na za msingi kwa jamii
inayozingatia
Sheria, pamoja na kuongezeka kwa thamani ya Ardhi kutokana na maeneo
kupimwa na
kupata hati milki.
Ongezeko la hali ya kiuchumi na kipato kwa jamii
kutokana na
kutumia hati katika kuomba mikopo katika asasi za kifedha. Manufaa
mengine
ameyataja kuwa ni kupungua na kuisha kabisa kwa migogoro na migongano ya
Ardhi
isiyokuwa ya lazima kutokana na kuzingatia Sheria na Mipango iliyowekwa.
Akitoa hoja, Mkurugenzi wa Manispaa
ya Iringa amesema ili kukabiliana na changamoto za kiutawala na
kiutendaji, ni
muafaka hatua madhubuti zichukuliwe kufuta vijiji vyote ndani ya eneo la
Halmashauri ya Manispaa ili kurahisisha utendaji na utekelezaji wa
mipango
endelevu katika maeneo yanayomilikiwa na vijiji kwa sasa.
