
Serikali imeongeza muda wa wiki moja kuanzia leo hadi Jumamosi ijayo ili kutoa nafasi zaidi kwa wananchi ambao watakuwa hawajafikiwa na zoezi la Sensa ya Watu na Makazi la Sensa lililokuwa linatarajiwa kumalizika hii leo.
Akizungumza leo na
waandishi wa habari jijini Dar es salaam Kamishna wa Sensa Hajati AMINA
MRISHO SAID amesisitiza kuwa muda huyo ulioongezwa hautaongezwa tena
hivyo wananchi ambao hawajahesabiwa watumie muda huo kuhesabiwa.
Hajati
AMINA amesema muda huo umeongezwa kwa kufuata sheria ya Takwimu Sura ya
Mia Tatu ibara ya Kumi na Nne ambayo inaruhusu kuandikisha watu hadi
muda huo uliopangwa.
Muda huo utaweza
kuwasaidia wananchi kupata fursa hiyo ya kuhesabiwa katika sense ya
mwaka huu.