Mkuu wa mkoa wa Iringa Dkt Christine
Ishengoma (wa tatu kushoto) akiwa na waumini wa dini ya Kiislam na
wakristo siku alipoandaa futari wakati wa mwezi mtukufu wa ramadhani
Ikulu Iringa
MKUU WA MKOA IRINGA MHE. DKT
CHRISTINE ISHENGOMA AMESEMA SENSA YA WATU NA MAKAZI INAYOENDELEA HIVI
SASA HAPA NCHINI HAINA UHUSIANO WOWOTE NA ITIKADI ZA DINI WALA CHAMA
KAMA AMBAVYO BAADHI YA WATU WANAVYODHANI.
MKUU WA
MKOA AMETOA KAULI HIYO LEO WAKATI AKIHOJIWA NA MWANDISHI WA MTANDAO HUU WA www.eddymoblaze.blogspot.com FRANCIS GODWIN,AMESEMA LENGO LA SENSA HII
INAYOENDELEA NI KUPATA TAKWIMU NA IDADI YA WATU KWA AJILI YA KUPANGA
MAENDELEO YA NCHI NA SI VINGINEVYO.
AMEWATOA WITO KWA
WANANCHI KUTOA USHIRIKIANO KWA MAKARANI WANAOFIKA KATIKA KAYA ZAO ILI
KUIWEZESHA SERIKALI KUPANGA MIPANGO YA MAENDELEO KWA WANANCHI WAKE
AIDHA AMESISITIZA KUWA ENDAPO KUFIKIA KESHO KUNA MWANANCHI ATAKUWA
BADO HAJAHESABIWA WATOE TAARIFA KWA VIONGOZI WA VIJIJI AU MTAA ILI
WAWEZE KUHESABIWA