TAZAMA JINSI AJALI YA MOROGORO ILIVYOKUWA

Picha zote na Danstan Shekidele, Morogoro Yetu

Askari wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Morogoro akipokea maelezo kutoka kwa abiria wawili akiwemo mwanajeshi waliokuwa ndani ya basi hilo la Allys lenye namba za usajiri T692 BKV ambalo lilikuwa likitokea jijini Dar es salaam kwenda jijini Mwanza 
 
 Afande wa kike anayefanya doria kwa kutumia pikipiki akiwasaidia watoto wawili kwenye gari ya polisi na kuwapekea kwa mama yao ambaye inadaiwa kuwa amejeruhiwa vibaya na kukimbizwa hospital ya mkoa wa Morogoro.
 Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Anthony Mtaka [kushoto] ambaye ajari hiyo imetokea kwenye Wilaya yake akifarijiwa eneo la tukio na Meya wa halmashuri ya Manispaa ya Morogoro Amir Juma Nondo [kulia]
 Abiria huyu Tatu Anthony akiangua kilio baada ya kunusurika kwenye ajari hiyo ambayo hakuna mtu aliyepoteza maisha
Abiria huyo akiwa na watoto wake wawili ambao wote walinusurika kwenye ajali hiyo 
 

Mama huyu alinaswa na mtandao huu akitoa mizigo yake kupita kwenye tundo la kuingiza hewa ambalo hukaa juu ya basi
 
 MMOJA wa abiri waliokuwa kwenye gari la Allys akimnyonyesha mtoto wake mchanga muda mfupi baada ya kuchomoka kwenye basi hilo
 

 Basi na Sumry lenye namba za usajiri T 777 BWL ambalo pia lilikuwa likitokea Dar kuelekea Mwanza nalo lilipofika eneo hilo hilo lilianguka huku sababu ikielezwa kuwa hiyo hiyo ya barabara kuteleza
 
 Gari ya wagonjwa la jeshi la polisi mkoa wa morogoro lilifanya kazi kuwakimbiza majeruhi hao hospital ya mkoa wa Morogoro


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo