NA
RIZIKI BONZUMA, MAKETE
Vikundi vya kuweka na kukopa
wilayani Makete vimeshauriwa kutobweteka na misaada kutoka kwa wa hisani
mbalimbali, badala yake wajitoe kwa kuchangia
fedha na vitu mbalimbali kwa ajili ya kusaidia watoto wanaoishi katika
mazingira magumu wilayani hapa
Akiongoza harambee ya
kuchangia misaada mbalimbali katika
kijiji cha Isapulano wilayani Makete mratibu wa mradi wa pamoja tuwalee
unaotekelezwa na shirikal la ELCT Makete Mchungaji Ezekiel Sanga amesema ni
wakati sasa wa wanamakete kujitoa wenyewe kusaidia watoto waishio katika
mazingira magumu lengo likiwa ni kusaidia watoto hao kutokosa haki zao za
msingi ikiwemo malazi elimu na chakula
Aidha katika harambee hiyo
iliyosimamiwa na shirika hilo
zimepatika fedha taslimu Tsh 80,000 na
zaidi ya debe 8 za mahindi ambazo
zitagawiwa kwa watoto kumi na saba waishio katika mazingira magumu kutoka
katika kijiji hicho cha Isapulano
Kwa upande wa wananchi
wakijiji hicho wameonekana kufurahishwa na na kitendo hicho na kuongeza kuwa
kisishie Isapulano tu bali kiendelee hata sehemu zingine za ndani na nje ya
wilaya ya Makete na kuomba watu wenye uwezo kujitoa ili kusaidia watoto hao
kwani kwa kufanya hivyo Mungu atawazidishia zaidi ya kile walicho nacho
