SIKU moja baada ya waziri
wa Afrika Mashariki na mbunge wa jimbo la Urambo Mashariki Samwel Sitta kumrushia kombora
mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na
maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe kuwa ,katibu mkuu wa Chadema Dkt
Willbroad Slaa aibua tuhuma nzito dhidi ya waziri
Sitta amwita msaliti .
Dkt Slaa amedai kuwa waziri Sitta
ndie alikuwa katika makubaliano ya
kuja kugombea uspika kupitia
Chadema ila alisaliti pamoja na kukubaliana vizuri kuwa angekihama chama chake CCM.
Dkt Slaa alitoa tuhuma hizo
leo mjini Iringa alipozungumza
na waandishi wa habari
katika hoteli ya M.R alisema ilikuwa Mei mwaka
2010, Sitta ambaye hivi sasa ni Waziri wa Afrika Mashariki alipokutana
na viongozi wa Chadema na kuonesha dhamira ya kujitoa CCM na kujiunga na
chama chao ila alionyesha usaliti
wa hali ya juu.
Alisema kuwa
katika mazungumzo hayo yaliyoendelea kufanywa katika kipindi chote cha
bunge la bajeti lililokuwa la mwisho kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka
2010, Dk Slaa alisema katika masharti yake ya kujiunga na Chadema, Sitta
ambaye kwa wakati huo alikuwa Spika, alitaka apewe nafasi ya kuwania
urais kupitia chama hicho na vikao vilikuwa vikifanyika ofisini kwake Dodoma.
Alisema ameamua kutoa siri hiyo baada ya
kiongozi huyo (Sitta) kunukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari juzi
akidai kwamba Dk Slaa ni mtu pekee ndani ya Chadema ambaye ni tishio kwa
urais katika uchaguzi ujao, huku akimponda Mwenyekiti wa chama hicho,
Freeman Mbowe kwamba ni mchezesha disco.
Hata hivyo
alisdai kushangazwa na waziri Sitta kuanza kuzungumzia mambo ya watu
badala ya kujibu hoja na kuwa
Chadema haipendi kuzungumza habari za watu, inazunguma maendeleo. Kwa
muda mrefu tumemuhifadhi Sitta lakini baada ya kupeleka mashambulizi
sehemu isiyohusika sasa tunampiga ngumi za tumbo na uso
Dkt Slaa alisema kuwa wakati
akitaka aandaliwe mazingira ya kujiunga na Chadema na kupewa nafasi ya
kuwania urais, Sitta alidai ana kundi la wabunge zaidi ya 55 waadilifu
kutoka katika chama hicho ambao angetoka nao pamoja CCM na kuhamia
Chadema kabla ya bunge kuvunjwa.
Alisema kwa kuwa Chadema haina ubinafsi,
ilihadi kuyafanyia kazi maombi yake ya kuwania urais kwa uzito mkubwa
hata hivyo katika mazingira ya kushangaza aliwatelekeza.
Dk Slaa alisema Sitta ambaye uzoefu wake
katika siasa na umakini wake katika kushughulikia maendeleo ya nchi
umeanza kuwatia shaka watanzania, alisahau jinsi alivyowatelekeza kabla
ya Uchaguzi Mkuu na baada ya uchaguzi huo akaja na hoja mpya kitaka
Chadema wampe nafasi ya kuwania uspika kwa kile alichodai kuwepo kwa
mizengwe ndani ya CCM.
Katika mazingira ya kushangaza badala ya
kufikia uamuzi wake wa kuhamia Chadema kama dhamira yake ilivyomtuma,
Sitta aliwatelekeza tena akidai kwamba atajiunga na chama hicho mpaka
pale atakapokwenda jimboni kwake Urambo na kutangaza rasmi kujiondoa
CCM.
Alisema kiongozi huyo
aliyekuwa akitaka msaada wa viongozi wa Chadema ili afanikiwe kujiunga
na chama hicho na hatimaye kupewa nafasi ya kuwania nyadhifa alizokuwa
akitaka ameanza kuwatusi hadharani viongozi hao akiwemo Menyekiti wake
Mbowe.
Alisema kauli
inayotolewa na Sitta kwamba Mbowe ni mchezesha disco inadhihirisha jinsi
asivyo makini jambo linalowafanya waanze kuitilia shaka elimu na uzoefu
alionao katika kuendesha shughuli za serikali.
“Sita anataka kutuambia kwamba watu
wanaocheza disco wakiwemo mawaziri wengi tu wanaokutwa kwenye kumbi za
burudani wanatenda dhambi na ni uhalifu kufanya hivyo?,” alisema.
Alisema kama biashara hiyo ya Mbowe
inafanywa kinyume na sheria za nchi, serikali inasubiri nini kufuta
leseni yake.
Kuhusu uongozi na namna
ya kupata viongozi ndani ya chama hicho, Dk Slaa alisema sio kazi ya
Sitta akuwapangia utaratibu.
“Sitta hajui kwamba duniani hakuna chuo
cha kusomea uwaziri, ukatibu mkuu, na hajui kwamba Mwalimu Julius
Nyerere hakuwa na uzoefu wakati akipewa madaraka ya kuongoza taifa hili
na kwamba hata wasaidizi wake nao walipata uzoefu baada ya kupata
madaraka,” alisema.
Alisema Sitta ni kiongozi mnafiki na
atakumbukwa zaidi alipokuwa Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania kwasababu kuna hoja mbalimbali zilizowasilishwa na wabunge wa
upinzani kuhusu ufisadi alizizima.
Alisema kuzimwa kwa hoja hizo ikiwemo ya
Mkataba uliogubikwa na utata wa Buzwagi, unadhihirisha jinsi naye
alivyotumia madaraka yake vibaya kwa kujenga ofisi ndogo ya Spika ambayo
yeye aliita ya mbunge jimbo kwake Urambo.
Alisema wakati serikali imeridhia ofisi
za wabunge zijengwe kwa kiasi cha fedha kisichozidi Sh Milioni 40 kwa
kuzingatia upatikanaji wa fedha, ofisi hiyo ya Urambo ilijengwa kwa Sh
Milioni 350.
“Kauli zinazotolewa na
Sitta kuhusu chama chetu zinadhihirisha jinsi alivyomnafiki na asivyofaa
jambo lililosababisha hata CCM wamemnyime nafasi ya kuwania kugombea
kwa mara nyingone tena nafasi ya Uspika,” alisema.
Dk Slaa na viongozi mbalimbali wa chama
hicho wako mkoani hapa, wakisubiri waanza mikutano yao ya vugugugu la
mabadiliko walilolipa jina la M4C baada ya kuzuiwa na jeshi la Polisi
kufanya mikutano yao katika kipindi chote cha sensa.
Wakati huo huo Dkt Slaa ameshindwa kutolea ufafanuzi juu ya kiasi cha fedha walizotenga
kwa ajili ya mikutano yao ya M4C inayoendelea
hapa nchi huku akiishia kudai kuwa fedha zinazotumika ni fedha zinazotokana na ruzuku ya serikali na michango ya wananchi bila
kutaja kiasi hicho cha fedha.