Mkuu wa wilaya Makete, Josephine Matiro
Na Edwin Moshi, Makete
Makarani watakaoshiriki zoezi la
sensa ya watu na makazi wilayani Makete wametakiwa kutenda kazi hiyo kwa moyo
na uaminifu mkubwa kama mafunzo yanavyosema ili taarifa zinazohitajika na
serikali kupitia zoezi hilo
la sensa ziweze kufanikiwa
Akizungumza wakati wa kufunga
mafunzo ya makarani wa sensa yaliyoendeshwa kwa muda wa wiki mbili wilayani Makete,
mkuu wa wilaya hiyo Josephine Matiro amesema anaamini makarani hao walipatiwa
mafunzo yao ipasavyo kama alivyoshuhudia wakati alivyokuwa akihudhuria wakati
wakipatiwa mafunzo hayo na kusema wao wanategemewa kwa kiasi kikubwa
kufanikisha zoezi hilo
Amesema endapo watakiuka mafunzo
waliyopatiwa kutapelekea zoezi hilo kutofanikiwa
hali ambayo haitegemewi na yeye pamoja na serikali kwa ujumla hivyo wanatakiwa
kutambua dhamana waliyokabidhiwa ni kubwa hivyo ni azima waifanye kama inavyotakiwa
Pia amewataka kupambana na
changamoto zitakazojitokeza na kuhakikisha wanatoa taarifa mapema kwa
wasimamizi wao mara moja pindi wanapokutana na changamoto ili ziweze kutatuliwa
haraka na zoezi la sensa liendelee
Kwa upande wao makarani hao
wamesema wanashukuru kwa mafunzo waliyopatiwa na wameahidi kuekeleza jukumu la
sensa lililopo mbele yao kwani wanatambua
dhamana waliyokabidhiwa hivyo wamemuahidi mkuu wa wilaya kuwa watafanikisha
zoezi hilo kama
inavyotegemewa na serikali
Zoezi la sensa ya watu na makazi
litatekelezwa nchi nzima kuanzia usiku wa 25/08/2012 kuamkia Agosti 26, mwaka
huu hivyo wananchi wote wanaombwa kushiriki zoezi hilo kikamilifu

